Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo 
Concepts Tanzania Limited, marehemu Vicky Mgoyo

Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania, Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.

Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhani Kibanike, alisema marehemu Vicky Mgoyo alifariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokimbimbizwa kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa usiku wa kuamkia leo.

Alisema kifo cha Vicky zaidi akijulikana kwa jina la Mama Mgoyo kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia yake bali pia kwa Kampuni ya Jambo Concepts kutokana na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu kazini, lakini pia uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzake.

"Tumepoteza mfanyakazi ambaye ni mchapa kazi na kipenzi cha wengi, tutamkumbuka kwa hilo. Naomba wafanyakazi tuungane na ndugu na jamaa katika kuomboleza msiba wa kipenzi chetu huku tukiamini kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

"Bado hatujapata taarifa rasmi za maziko, ila taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao zinaendelea kufanyika," alibainisha Kibanike.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pinto alitoa mwito kwa wafanyakazi kuonesha mshikamano katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao.

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwesa, akizungumzia msiba huo alisema Mama Mgoyo ametwaliwa na Mungu ilhali akiwa bado anahitajika na familia pamoja na ofisi yake, hivyo ameacha pengo ambalo litachukua muda kuliziba.

"Mwenzetu ametangulia nasi tupo nyuma yake, zaidi tumwombee ili Mungu ampumzishe katika raha ya milele," alisema Mwesa.

Kwa upande wake Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hilo, Richard Mwaikenda, alisema atamkumbuka Vicky kwa kuwa ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa anazingatia maadili ya kazi yake ya uhasibu.

Pia alisema alikuwa ni mama mjane makini ambaye alihakikisha anasimamia watoto wake katika suala la kuwapa elimu bora, ambapo katika hilo alikuwa akifanya kila anachoweza kuhakikisha anasomesha nje ya nchi tena kwenye shule bora na makini.

Vicky Mgoyo aliyezaliwa Novemba 26, 1964, ameacha watoto watatu huku wawili kati yao ni wanaume.

Alilazwa katika Hospitali ya Kairuki wiki iliyopita ambako alipatiwa matibabu kwa muda wa siku nne na kuruhusiwa.Jumatatu aliripoti kazini na kuendelea na kazi hadi jana jioni, ambapo usiku alizidiwa na hatimaye leo asubuhi Mungu alimchukua. Mungu ailaze pema peponi roho ya Vicky Mgoyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2013

    Poleni sana wafiwa. Hivi wanawake wanaoitwa Vicky huwa na tabia zinafanana: Wachapa kazi, waaminifu kazini, uchashi, full furaha....

    Nakumbuka kuna mama mmoja pale UCC CHUO KIKUU aaaaaaaaa!Huyu mama hata ukiwa na shida gani iliyo ndani ya kazi yake , itamalizika tu. Sisi wanafunzi tuliowahi kusoma pale, ukipoteza risiti hata kama ya miaka 3 iliyopita, ukienda kwake, kama hatapata risiti kuna mahali ataona pa kuonyesha kuwa ulishalipa , na atakuandikia kikaratasi utapeleka kunakohusika.

    Lakini bahati mabaya utenaji huo mzuri ulimponza, nilikuja kupata taarifa kuwa bosi wake ktk kuona kuwa utendaji huo unamkosesha ulaji akamuanzishia bonge la manyanyaso, mama wa watu akapisha soo.

    Huyu Vicky aliyefariki amenikumbusha mengi. Poleni sana wafiwa, na mwajiri wake pia

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2013

    Inawezekana ni kweli akina Vicky ni wachapakazi wa kweli, mm nilifanya kazi na mmoja aliyekuwa Benki, siwezi kusema kitu juu yake nikawa nimesema sawasawa, ila alifanya kazi yangu iwe nyepesi pamoja na kuwa nilikuwa ndiyo kwanza nimeajiriwa wakati huo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2013

    Ehe! kumbe huyu mama wa chumba namba 5 UCC alishaondoka! nimeskitika sana. Lakini asingeweza kukaa ka kuwa Bosi mkuu pale nasikia hataki kabisa mfanyakazi asiyejua wizi.

    Nawataarifu wanafunzi wenzangu mkipewa risiti na yule mzee mnoko wa pale dirishani ucc itunzeni vizuri. Huyo mzee hatari..Kwanza ukifika pale anakukunjia uso utafikiri anaku.....

    Ukimlipa fizi untaambiwa mtandao haupo njoo kesho, kesho yake humkuti . Na siku zinavyozidi kwenda na uwezekani wa kupata risiti yako ni ngoma.

    Sasa sikiliza kivumbi wakati wa kumaliza kozi utaambiwa hujamaliza fizi.
    Huna mahali pa kupata risiti ndo inakula kwako

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2013

    Hawa jamaa nao hawana dogo...Mimi ilinikuta nikajuta kujiunga pale.Mie nilipangwa kusoma tawi la mbezi, Yule mdada wa mbezi akaniambi niende chumba namba 5 makao makuu wahakiki slip yangu ndio nirudi kuandikiwa risiti

    Bwana wee nikamkuta mdada mwingine mweupe hivi akaniambia:sina nafasi naenda kula.nisubiri nikirudi.Nilikaa pale tangu saa 7.30 paka saa 10 aliporudi.Eh bado upo! ananishangaa. Nani aingie kwenye mafaili saa hii? aliuliza mdada amevalia suruali iliyobana sana.
    Nipe karatasi hiyo nitaangalia kesho ukirudi utakuta tayari.Alisema kwa mikogo.

    ilibidi niache slip pale na kesho yake nilienda sikumkuta , wenzie walisikika wakisema kuwa leo ajajisikia kuja.

    Jamani.Namna hii tunatesana.Fee tulipe na mateso tupate

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...