Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.

Mpaka sasa ushirikiano tulioupata ni kampuni ya Clouds Media Group ambayo imebeba jukumu la kusafirisha mwili wa marehemu kutoka South Africa mpaka Tanzani, Bongo Records wameshachangia shilling milion 5 na Push Mobile wametoa million 5. 
Kamati inaomba wizara husika, mashirika, makampuni pamoja na watu binafsi kutoa michango yao katika kukamilisha jukumu la kumhifadhi katika nyumba yake ya milele ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha.

Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:

Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738

Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanguliza shukrani za dhati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2013

    Mchango gani zaidi jamani?????, mbona tunataka kumega dili juu ya bega la mswahili?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2013

    clouds group washajitolea kuleta maiti, bongo records mil, 5 na mwingine sijui mil 5. KWELI MNATAKA SEMA MILIONI 10 HAZITOSHI KUPELEKA MAITI TOKA DAR-MOROGORO?????

    KUFA KUFAAANA....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2013

    Hivi jina kumbe ni Mangweha manake siku zote mnaandika Mangwea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...