Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bwana William Erio amechaguliwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka wa kampuni ya Zep-Re kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kampuni hiyo. Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Mkutano Mkuu huo uliofanyika jijini Mombasa, Kenya tarehe 10 Mei mwaka huu.
Bwana Erio, ambaye atashika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 3, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Gavana wa Benki Kuu ya Zambia, Dr. Michael Gondwe aliyemaliza muda wake.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo wanatoka katika nchi za Kenya, Rwanda, Djibouti, Eritrea, Zambia, Sudan, PTA Bank na African Development Bank.
Zep-Re ni kampuni ya bima mtawanyo kwa nchi za PTA yenye makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya na ina ofisi ndogo katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Sudan na Cameroun
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...