Napenda kukumbusha kuhusu mjadala mkubwa na wa kihistoria wa waTanzania utakaofanyika 3Sixty, University of Reading, siku ya tarehe 01/06/2013. Kwa taarifa tu, kutakuwa na usafiri kwa wale watakaohitaji. Usafiri wa basi utaanzia London saa 4:00 (nne kamili) asubuhi. 
Kama unahitaji huduma hii unashauriwa kuwasiliana na Bernad Irondo kwenye namba hii: 07804804963 kabla ya siku ya Jumatano tarehe 28/05/2013. Kwa hisani ya Funguka Forums, mjadala utakuwa unachukua maswali live kupitia Tweeter (@fungukaforums). 
Pia updates za mjadala zitakuwa zinarushwa live kwenye www.fungukaforums.com , facebook (www.facebook.com/funguka.fungukaforums). Pamoja na facebook, mjadala utaruhusu ushiriki kwa kupitia Skype (funguka). Hii ni kuwapa nafasi ya kushiriki wale wote wakakaoshindwa kuhudhuria siku hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Haijalishi mahali ulipo, shiriki kwa kupitia Tweeter au Skype ama fuatilia kwenye forum au facebook. 
Hata hivyo kama hutahudhuria ila una mchango wako unaogusa moja ya topic zitakazozungumzwa siku hiyo tafadhali tuma swali/maoni kwenye email: team@fungukaforums.com. Maswali yote yatakusanywa na kusoma wakati mjadala ukiendelea. Karibuni wote na umkaribishe/mjulishe mwenzako.

G Mboya
Secretary
CHADEMA UK 
(+44)(0)7846783365 (m)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    kwanza tarehe na siku haviendani.

    pili ni twitter na sio sijui nini umeandika.

    sad mtu ulaya au hukwenda kussoma maana mmh makosa hayatakiwi katika haya, muwe mbarudia kusoma mlichoandika kuona kma mambo yapo sawa.

    Mdau sina chama

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2013

    Mdau wa kwanza kabisa hapo juu. Je, wewe mwenyewe binafsi UMEIRUDIA hiyo habari yako uliyoiandika ili kuona kama mambo yapo sawa? Isijekuwa kuchekana kwa Manyani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...