Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi (kulia) akipokea Tuzo za Bia Bora Afrika ambazo Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilishinda katika Mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tuzo hizo zitatembezwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa siku mbili. Anaemkabidhi tuzo hiyo ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi wakinyanyua Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tukio hilo lilifanyika jana katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya Safari Lager ambapo zitatembezwa katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo kwa siku mbili.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Raymond Mushi akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye eneo la wazi la Ilala Mchikichini kushuhudia Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager.
Wakazi wa jiji la Dar wakiwa wamefurika kwa wingi kushuhudia Kombe hilo la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika Ulioupata Bia ya Safari Lager.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...