Na Abdulaziz,Lindi
Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Sudi Ahmad Lilah (24) mkaazi wa Kitomanga
wilaya Lindi amefariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya
gari aina ya Isuzu Tipper yenye namba za Usajili T441AMC iliyotokea
kati ya kijiji cha Mkwajuni na Namkongo wilayani humo saa Sita za
Usiku kuamkia leo.
Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Kilombilo Eliana Mariki ambalo
lilibeba Tofari kwa ajili ya kupeleka katika ujenzi wa kisima cha Maji
Namkongo tofali ambazo zilitoka katika kijiji cha Mitwero limepata
ajali hiyo na kuporomoka katika bonde na Tofali hizo kuufunika Mwili
wa marehemu alifariki hapohapo
Kufuatia taarifa ya awali ya Muuguzi wa zahanati ya Namkongo Bi Regina
Blasius na Kuthibitishwa na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Lindi,Renatha Mzinga zinaeleza kuwa Majeruhi wamefahamika kwa Majina
ya Godbless Mgati(21) mkazi wa wailes lindi,Juma Abdulrehman(24)mkazi
wa Ndoro na Hassan Masudi(28) Fundi bomba mkazi wa Makonde
wamefikishwa asubuhi hii na kulazwa kwa Matibabu zaidi katika Hospital
ya Rufaa ya Sokoine Mjini Lindi.
Marehemu Sudi alikuwa katika gari hilo kama mchukuzi wa kupakia
na kushusha tofali hizo. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospital hiyo ambapo ndugu na jamaa wameombwa kujitokeza kuitambua pamoja na kuichukua kwa mazishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...