Kwanza shikamoo mzee wa libeneke na wadau wote walionizidi umri.
Mie ni mdau mkubwa wa blog hii inayosomwa kwa wingi duniani leo nineona nami niombee msaada wa mawazo km wasomaji wengine wanaotoa matatizo yao na kupata msaada wa mawazo.
Mie ni kijana mwenye umri wa miaka 30 naishi norway kwa sasa ila ki ukweli kwa miaka 7niliyoishi hapa sijafanikiwa kupata makaratasi kifupo niko illegal nilijiripua km vijana wengi tufanyavyo na majibu ni negative. Sasa bahati ya Mungu nimecheza bahati nasibu ya green card ni nimefanikiwa kuwa mmoja wa waliochaguliwa, natakiwa kujaza form na kufanya interview ambayo itafanyika Dar, Mungu akipenda, mimi kwa kweli mpango wangu nilikuwa sirudi bongo mpaka kieleweke huko as nimeshapoteza muda mwingi, je wadau najua kuna waliowin green card, how sure it is to get a visa?.
Naweza kweli kupata visa au naweza rudi nikaganda? Mnanishauri nirudi?
Naomba msiwe wakali sana maisha magumu ndo yamenifikisha hapa.
Asante ankal, email kapuni please.
Davis

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 63 mpaka sasa

  1. SolicitorMay 07, 2013

    Kwanza hongera mdogo, siyo kwa kushinda green card, bali kwa kuwa shujaa katika kutafuta maisha. Kwa kuwa umesema ulijilipua, basi tegemea matusi na kebehi kwa wale ambao wangependa kuishi ughaibuni lakini wameshindwa kwa namna moja au nyingine.

    Sasa kwenye hili suala lako la green card, kama utapata visa au hutopata; inategemea na wewe mwenyewe kama ulipoomba hiyo bahati nasimu ya green card ulisema ukweli na uongo kiasi gani.
    Kama ulisema kweli tupu, basi hakuna sababu ya wewe kukosa green card visa.
    Kama ulisema uongo mwingi, basi inabidi uweze kuutetea uongo wako hapa ubalozi wa marekani wa bongo.
    Lazima watakuuliza mambo kama
    1. Ulipoomba green card ulikuwa nchi gani, ulikuwa unafanya nini, kama uliwahi kufanya kazi, uzoefu wako wa kazi, elimu yako, na kadhalika. Maswali mengi yatakuwa tuu kwa ajili ya "identity verification" na "identity fraud prevention".
    Lakini pia ndani ya maswali hayo kutakuwa na maswali ya mitego kujua kama wewe ni mtu safi.

    Kama huwezi kujitetea basi komaa Norway mdogo wangu, miaka 7 ishapita basi baada ya miaka michache tuu utapewa pasipoti yako ya Ulaya. Nchi nyingi za Ulaya zina sheria kwamba ukikaa baada ya miaka fulani, basi unatakiwa upewe makazi. Lakini hili nalo linategemea kama huna matatizo na polisi wa Norway.

    Duh! ningekuwa bado nipo UK, haya niliyoyaandika hapa yanaitwa "initial consultation" na ningeku-charge kama £70 hivi.

    Mdau, solicitor.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2013

    Ndugu yangu umeishajilipua bakia hivyo - labda oa Mnorway - sijui sheria za ndoa na immigration zikoje. Mimi na familia yangu tuliingia Marekani kihalali kwa kushinda visa - kitendo cha kuambiwa urudi home ufanye interview? Utajielezaje kwa muda uliokaa illegally? Ushauri wangu endelea kulipuka

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2013

    Davis, interview za green card ni formality tu wewe ni mshindi wa hiyo green card piga ua utapewa, ni aghalabu sana kudundisha yaani sijui uwe zezeta kiasi gani, kwa miaka saba uliyoishi ulaya naamini kabisa umejifunza mengi mno walau hata jinsi ya kujielezea binafsi.Kinachonitatiza kidogo ni kwamba iwapo utaulizwa vitu kama personal number,address kwa maana ni vitu muhimu pande hizi kwa mtu anayeishi huku iwapo ulikaa huku kwa kipindi chote hiko. Vinginevyo kila la heri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2013

    Mdau kwanza hongera sana kwa kushinda greencard. Nenda kwenye website ya serikali ya USA uthibitishe kama kweli umeshinda. Uzuri wa wenzetu wamarekani wakikueleza kuwa umeshinda, basi ujue ni kweli. Hawana usanii hata kidogo. Rudo bongo kapige interview yako kiulani na wala usifikirie kukataliwa, labda kama umewahi kujihusisha na masuala ya kigaidi. Njoo unyamwezini hapa na uanze kufaidi matunda ya kadi yako. Wewe na mwenzako wa ndoa mtafanya kazi kihalali na mkita shule ngazi yeyote serikali ya USA itawalipia. Baada ya miaka 5 mtapata uraia. Good luck.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2013

    ndugu kuna issues nyingine, hasa hii ya visa affairs huwa ni za kibinafsi zaidi, kama kweli umeshafika mtoni mambo mengine ni akili yako mwenyewe. Vinginevyo labda unataka kuona comments za ajabu ajabu hapa blogini. Kweli wabongo sasa duniani tumekuwa ni vituko, mambo kama haya watu sasa wanaamua kuanika hadharani kuomba ushauri wa watu? sitoshangaa mtu km wewe ukaenda hata kuuliza nchi husika ya ughaibuni officially kuwa eti hivi sasa nijiripue kivipi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2013

    Tumia Akili vizuri ila tunakuombea Mungu ufanikiwe. Mliopita hizi nafasi za Green card msaidieni mwenzenu Dunia hii yangu mungu hakuna mwenye yake kuishi kokote kule maisha popote kutapokukalia sawa ww ila ndugu yangu kila mafanikio nakutakia ila ushauri wangu kama ni Norway ukipata Stay au kama ni USA usisahau kusoma Elimu ya Akhera na ya Dunia na tulizana na maisha.. M

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2013

    Kama ni USA green card utaipata kama umetimiza masharti yote ya green card, kama medical check-up, visa fee, na kama kuna mtu atakupokea na utaishi naye utakofika Marekani..utatakiwa kuwa na mtu huyo na address yako ni hivyo, jua kwamba ni gharama kidogo...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2013

    KUNA FRIEND WANGU ALIKUA ANAISHI INSTABUL ALISHINDA GREEN CARD AKATAKIWA KURUDI BONGO FOR INTERVIEW LAKINI AKAANDIKA BARUA UBALOZI WA USA ( TURKEY) WAKAMKUBALIA KUFANYA INTERVIEW INSTABUL.... JARIBU FATILIA KIUNDANI NDUGU USIRUDI BONGO UKAKAA KIJIWENI HALI NGUMU.. GOOD LUCK

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2013

    Hali yako ni ngumu kidogo ila kama ulifanikiwa kusevu kiasi cha kutosha kuhonga pale airport na immigration kusudi upate makaratasi halali ya kitanzania yasiyokuwa na shaka yoyote, na huko uliko hujawahi kupatikana na hatia yoyote ya kufikishwa polisi, basi utafanikiwa tu. Green Loto interview huangalia zaidi tabia yako nchini kwenu kwa vile huwa wanategemea kuwa hujawahi kuhamia nchi nyingine.

    Hongera sana

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2013

    Mwanangu nimekukubali yaani wewe ni kamanda, umefanya vizuri sana kuuliza bila kukurupuka. Kiukweli naamini utasaidiwa tu na haswa ndugu zetu waliopo AMERICA Watakupa mawazo mazuri humuhumu ndani ya blog cha msingi usikurupuke kwanza kurudi bongo inabidi ujiridhie nafsi na akili ili kama mambo yakienda ndivyo sivyo usiteseke kisaikolojia. GOOD LUCK BRO!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2013

    USA Hamna mpango stress za kuua Mtu Huku ataukiwa na green card mambo yale Yale .wewe bakia Norway tafuta mke Uko .

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2013

    Pole ndugu yangu. Mambo ya makaratasi. Nakushauri jaribu huko uliko Ila ukirudi bongo uwe na mawili kupata au kukosa. Maisha popote kama umeshidwa kwa miaka saba kama ni kweli pole sana

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2013

    Green Card ni ukweli kama umepata unatua Marekani bila matatizo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2013

    Wewe nikupe wazo zuri tu - acha kuhangaika. Tanzania ya sasa si ya Zamani. Kuna opportunities nyingi tu na in fact watu wa nje wanakuja nchini wakati nyie mnakimbia!! Na gesi itafumuka hivi karibuni. Utangaika na nchi za watu mwishoni utajikuta UMEZEEKA.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2013

    Greencard lottery ukishashinda inabidi uombe viza. Masharti yake kwa aliyeshinda si magumu uwe umemaliza alau Form VI. Au amewahi kufanyakazi kama Engineer, Mwalimu wa Biology, na kazi zengine kwa miaka miwili katika mitano iliyopita. Kama huna hizo option mbili basi itabidi utulie Norway usibiri msamaha wa serikali kwa watu waliojiripua muda mrefu. Pia jaribu kutafuta mwanamke uzae nae. Au fuga mbwa au paka pia unaweza kuruhusiwa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2013

    Kwanza hongera sana.

    Niandikie email binafsi; malynnib kule katika yahoo doti com. I am looking forward to guide you further through the process.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2013

    Unajua, huyu bw. mdogo jinsi alivyojieleza ananikumbusha japo si moja kwa moja sana, kile kisa cha mwana mpotevu (katika biblia) aliyerudi kwa babaye na kusema "sistahili kuitwa mwanao, nifanye kuwa mmoja wa watumwa wako" yaani kwa kusema hivyo alitambua kosa lake na kujaribu kuwa mnyenyekevu ili apate msaada....na kweli akasaidika!

    Japo mie si mjuzi sana wa maisha ya ujanja ujanja kama haya yaani "kujilipua" n.k. kama alivyoita huyu mdau....lakini nadhani huyu bw. mdogo amejaribu kwa kiasi fulani kuwa muwazi na hivyo ikiwa uovu pekee alioufanya ni huu wa kujilipua ambao at least ameweka waji, nadhani hata mimi kibinadamu najisikia kumuombea mambo yake yamnyooke ili dogo aweze kutoka.

    Sijajua atawezaje kudadavua maoni hayo yote ya wadauz, ili apate muelekeo angalau sahihi lakini sasa hapa nadhani ndo wanasema waswhili "akili mu-kichwa"

    Upande mwingine, napenda kuwapongeza wote waliojaribu kutoa mawazo yao ili kumsaidia bw. mdogo (japo hii haimaanishi kuwa kila wazo hapo linaweza kuleta matokeo mazuri).

    Vyovyote vile, jambo la msingi unalotakiwa kujua dogo ni kuwa pamoja na ushauri wote huu wewe binafsi ndiye utakayewajibika na consequnces za maamuzi yako....All the best!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2013

    MAN achana na na watu wababaishaji....My name is Frank...call me @+18583665733...i am a Tanzanian and a greencard winner living in USA.I won when i came here..my process would be different but i can help..call me NOWWWW...you dont have to worry wewe umeshinda utafanikiwa TU tena vizuri kama uko nje ya marekani........SPEAK with me or check me on my facebook...https://www.facebook.com/frank.daniel.5815...email me here : official08@live.in,,.....YOU CAN TEXT BEFORE calling

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 08, 2013

    TATIZO NILIONALO MIMI NI KWAMBA US EMBASSY PAMOJA NA MAMBO MENGINE WATAHITAJI POLICE REPORT TOKA KILA NCHI ULIYOISHI ZAIDI YA MIEZI SITA BAADA YA KUFIKISHA UMRI WA MIAKA 18. KAMA UNA UHAKIKA UTAPATA HIYO REPORT NA ITAKUWA NZURI UNAWEZA KUJARIBU LA HASHA WASWAHILI USEMA NDEGE MMOJA ALIYE TUNDUNI ANA THAMANI ZAIDI YA NDEGE WAWILI WALIO ANGANI...BAKI NORWAY MPAKA KIELEWEKE.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2013

    Haa kuzaa ana kazi gani ya kumudu kulea mwana na mamaye! hapo alipo illegal kashasema! omba shule au subiri msamaha wa serikali ka ulivoambiwa dogo! yaani kama kuna kauwongo tu katajitokeza utaganda best! hawa jamaa hawana msheso!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2013

    Hongera kwa kushinda Green Card.

    Kuna jirani yangu kashinda Green Card, yeye hajamaliza Form V1, form Four tu. Mume wake alikuwa anaishi bila ya makaratasi Marekani. Wote wakapewa green card hapa hapa Bongo na walikuja mwaka jana kutembea na pasi yao ya Kimarekani.

    kwa ufupi, ujue tu haki yako na umetimiza masharti yao. Usiogope kugombania haki yako. Kuna tabia ya Watanzania wenzetu ubalozini ambao wanajifanya wao kama ni ofisa wa Kibalozi, wana roho mbaya. Kuna mama wa kihindi pale, asikutetemeshe kabisa, yeye anajitia balozi. Una haki ya kuomba kumwona afisa wa Kimarekani kama anakuzingua.

    Kuishi bila ya makaratasi Norway sio issue kabisa. Kuna Wapakistani Marekani walikuwa wanaishi kiholela na Bush alipoanza kuwatia ndani wasio na viza, wakakimbilia ukimbizi Canada na wengi wakapanchi. Kwa hivyo, kama umechaguliwa, utapewa viza yako, na familia yako yote. Hongera.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2013

    kaka ongera sana. mimi nakushauri usirudi kabisa. baki huko mpaka kieleweke. kwa maana ukurid bongo watakuuliza norway ulikuwa unafanya nini halafu watakuomba uthibitishe norway ulikuwa unaisha ki vipi kwani wamerekani hauwafaamu? yaani ukirudi bongo imekula kwako.....

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2013

    Ndugu,

    Hapa kuna watu wanajifanya ujuaji lakini naona watakuponza. Kuna vitu vya kuzingatia ukishinda greencard, kwanza it does NOT mean kuwa utapata hiyo viza. Kigezo kikubwa kinachotumika pia ni kitu kinaitwa viza number, swali la msingi namba yako ni ngapi? (usiiweke humu). Kumbuka viza zinatolewa 50,000 tu kwa mwaka, na kila bara lina quota yake. Namba za washindi (wanaotaarifiwa) huwa ni zaidi yazile viza 50,000, maana yake kuwa kuna wengine wanaweza wasirespond, au kushindwa vigezo, au muda wa kuprocess ukaisha (yes, kuna time frame ya kuprocess hizo greencard kwa mwaka).
    Laiti ungekuwa tayari ndani ya US, basi kuna kitu wanaita CoS (change of status), ungeweza kuifanyia humo ndani, ingawa process yake ni ndefu kidogo, kuliko kwa wale walioko nchini mwao (say Tanzania).
    Nadhani mpaka hapo umeshaona uko katika mwelekeo gani. Ila kuna mtu ninaye mfahamu binafsi, alirudi bongo kuja kuprocess GC yake, mpaka leo hajaondoka (mwaka wa nne sasa).

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 08, 2013

    msaidieni jamani

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 08, 2013

    Based on wewe kujilipua na kuwa Norway illigally, kitendo hiki cha kuwa mvujifu wa sheria basi moja kwa moja unaleta picha kuwa haufai kupata visa, hii ni most likely. wewe endelea tu kujilipua usijeishia kujinyonga ukirudi.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 08, 2013

    Mzee kuna mtu hapo juu amekumbushia kitu cha maana sana, hapa ni lazima kwenye interview watahitaji Police report ya nchi ulizokaa zaidi ya miezi Sita ili kujua kama ulifanya makosa ya jinai au la? Sasa hao Norway wanaweza kukupa hiyo report wakati wewe ni Illigal? fanyia kazi hili kama inawezekana unaweza fikiria kuja au la?

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 08, 2013

    MIMI NIPO LONDON KWA MIAKA 21 SASA.RAFIKI YANGU ALIKUWA HAPA KWA MUDA WA MIAKA 10.ALIKUWA AMEJILIPUA LAKINI HAKUFANIKIWA,BAHATI NZURI AKASHINDA GREEN CARD AKARUDI BONGO KWENYE INTERVIEW,KULE BONGO WALIMKATALIA ETI ALIKUWA ANAISHI UK BILA VISA,PILI ALIAMBIWA YEYE SIO RAIA MWAMINIFU.KWASASA NI MIAKA 5 IMEPITA YUPO BONGO KIJIWENI.NAMWAKA HUU JANUARY 2013 ALIKUWA ANATAKA KUJIUWA AKAOKOLEWA. USHAURI WANGU KWAKWO,MIAKA 7 ULIOKAA NI MINGI USIONDOKE UTAFANIKIWA.MVUMILIVU HULA MBIVI.MDAU CHELMSFORD.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 08, 2013

    Nchi ya norway ni nchi ngumu sana kuzamia,hongera sana,umewezaje kujilipua??maana norway ukiumwa uwezi kutibia mpaka uwe na personal number..kazi uwezikupata mpaka uwe na personal namba..kila kitu unaulizwa namba yako,nakushauri kama umefanikiwa kukaa norway bila tatizo nakuomba usirudi bongo....naomba tuwasiliane maana na mie nimekaa norway naijua vizuri sana,nimekaa hapo miaka 6

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 08, 2013

    Nenda stockholm kaongee na balozi wa scandinavia atakupa ushauri ni mtu mzuri sana...vinginevyo tuwasiliane

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 08, 2013

    Kupata Visa baada ya kushinda GREEN CARD ni pata potea!

    Kuwa na msimiamo pia huko NORWAY ulipo sio pabaya komaa, kama huna kazi nenda kavue samaki Bahari ya barafu.

    Zaidi ya hapo kama vipi jiamini RUDISHA MPIRA KWA KIPA, (yaani rudi nyumbani Tanzania) kwa kuwa kama Mdau mmoja hapo juu alivyosema Tanzania ya sasa sio mbaya kivile ukizingatia huko tunakoelekea kwa kuwa tuna Gas na Mafuta yaliyofumuka, ukihangaika nchi za wenyewe utapoteza muda na UTAZEEKA bure.

    Mtikisoko wa Uchumi Duniani:
    Eurocrisis na Global Financial Crisis kama ulivyosikia.

    -Ulaya wengine kazi za maana kama miaka ile hakuna sasa, wengi tu wanavuna matunda Mashambani!

    -Jamaa alikuwa anawasiliana na jamaa yake Marekani mara ka mara jamaa ana biashara zake Bongo akaenda Marekani kwa matembezi, cha ajabu yule mshikaji USA aliposikia jamaa amekuja akakimbia mji mwingine !,,, kumbe jamaa ktk USA yeye ni Mkazi wa Mitaani (homeless na anaishi kwa mafao ya jamii)!!!

    Mimi ninao jamaa nafahamiana nao walishinda Green Card zao wakaenda Marekani miaka hiyo (1900's -2000's) huko kulipokuwa na maisha ya ukweli lakini walipokuja Bongo matembezi waliona fursa kibao nchini na sasa wamerudi TZ na wanapata maisha bomba tu!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 08, 2013

    Dogo kuwa na msimamo!

    Chagua moja:

    1.Kuoa ama kuolewa huko Norway.
    2.Waombe uombee visa ya USA huko.
    3.Fanya kazi zavibarua uchume pesa.

    MAMBO YANABADILIKA KILA KUKICHA BONGO, MICHONGO YA KUINGIZA UWEZO WA KULA 'DONA NA MBAAZI KAVU' ULIYOIACHA KIPINDI ULIPOONDOKA MIFEREJI IMEZIBWA KITAMBO TU.

    UKIJA SASA UNAKUWA NDIO KAMA UMEZALIWA LEO!, UNAKUWA GIZANI TOTORO!

    Visa yenyewe ya Norway uliipata kwa bahati tu, kama hujui wazungu wana mipango sana Mwanawane, wamesha wasiliana wao kwa wao wewe hujui (USA na NORWAY), wakapanga uambiwe kuombea visa TZ ili ukiingia goilini mara hii kwa Mnyamwezi mwenyewe BIG BROTHER unatoswa!

    umeona akili hiyo?

    BAKI NORWAY !!!

    UKIRUDI BONGO UTAMEZWA NA MAMBA!

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 08, 2013

    Hongera kwa kushinda lottery. Kuwa mwangalifu sana. Mimi nakaa nje ya Tz. Kila nilipoenda kuomba visa ya kwenda nchi nyingine kutoka hapa, nchi hiyo imetaka kujua kama kuishi kwangu hapa ni halali ama haramu. Lazima wanaomba kuona PERMIT OF STAY ya hapa ninapokaa kwa sasa. Kama record yangu ni mbaya hapa, basi wanajua kuwa uwezekano wa record yangu kuwa mbaya katika nchi yao utakuwa mkubwa. Kwa hiyo wanakunyima visa yao. Hakuna shaka kuwa kama uliweka anwani yako kuwa ni Norway wakati wa kuomba, basi US Embassy in Dar watataka kujua kama ulikuwa unaishi kihalali Norway ama la. Wakijua kuwa ulikuwa unaishi haramu Norway, basi sahau hiyo Green Card Visa.

    Kama wakati wa kuomba uliweka anwani ya Tanzania na passport yako ikaonyesha kuwa hukupata kutoka nje basi rudi Tanzania ukapate Green Card Visa yako. Lakini chunga sana wakkati wa kutoka. Kuna uwezekano wa kukamatwa na kuwa detained na Maofisa Uhamiaji wa Norway kwa ku-overstay au kitu kingine kinachofanana na hicho.

    ReplyDelete
  33. Hongera sana kwa kujilipua na viza ya USA. Hiyo umekwishachaguliwa. Hakuna tatizo. Rudi nyumbani, tafuta pasi mpya kabisa ambayo haionyeshi rekodi zako za nyuma. Utapata viza na kwenda kutanua USA. Mwenda bure si mkaa bure. Kila heri.

    CCM UK

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 08, 2013

    Mimi nakushauri ufanye mpango wa kufanya interview ukiwa huko huko Norway kabla ya kurudi bongo..unaweza kwenda ubalozi wa USA in Norway wakupe utaratibu wa mtu aliyepata Green card nje ya nchi yake anawezaje kufanya interview akiwa hapo hapo kwenye nchi hiyo..usirudi bongo kwanza mpaka umejihakikishia kwamba utaweza kurudi tena Norway incase something goes wrong

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 08, 2013

    Mambo ya VIZA HAYANA UJANJA WALA KUJUA SHERIA ni BAHATI TU. Bahatisha bahati yako kama ulivyofika Norway, tena usiwe na huzuni, kimenuka unaanza maisha Bongo safi kabisa tena kuwa na furaha. Mfano viza ya UK huwa wanasera kuwa kila mwaka watoe viza idadi fulani, idadi ikifika wanatoa sababu yoyote ili kukukatalia viza. Pia anayeshughulikia faili lako anategemea ana itikadi gani. Kuna watu UK hawapendi kuona watu wasio raia halisi wanaishi pale hivyo hutafuta sababu kutunga sera mpya.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 08, 2013

    ohooo !

    wewe mtoto simba huwa anachezewa sharubu zake?

    uliipata viza ya Norway wakati wazungu walikuwa wamelala, hivi sasa wabongo wamechafua sana huko majuu na mabalozi yanabana sana watu.

    wewe kama huamini jaribu uone, urudi uje uombee visa hapa bongo uone kama utapata!

    nakuaminia safari hii ni lazima utalaliwa tu, utajikuta unabaki Bongo huku uchumi ukiwa umeyumba ukiwa na kazi kama hizi:

    1.Utakuwa Kinyozi Saluni,
    2.Utakaanga mihogo,viazi na samaki,
    3.Utakuwa Kondakta wa Daladala,
    4.Utaendesha Bodaboda,
    5.Utakuwa Kishoka wa TRA kutoa TIN ama UHAMIAJI kutoa PASIPOTI.

    Baki Norway matokeo yake utakuja omba visa ya Marekani hapa Bongo utadundishwa halafu Norway utajikuta huwezei kwenda tena kwa kuwa hadi sasa upo nje ya Sheria!

    Angalia utazama kaburini,

    Utakosa KOTEKOTE,

    Shauli zako!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 08, 2013

    Wewe motto acha ujinga wako!

    Watu wamenasa Bongo wanashindwa kuchomoka wewe unachezea bahati?

    Kaa Norway hata kama huna kazi utakula Kanisani, Ustawi wa Jamii ama Serikali za Mitaa na Huduma za Jamii (SOCIAL SECURITY) za bure huko unapata licha yakuwa upo nje ya Sheria.

    Sasa Bongo ni wapi nieleze utapata, Hela ya kujikimu Maisha ya bure ama Dona la bure?

    Bongo dishi la bure uwe Gerezani ama siku ya Sherehe tena kwa Kadi.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 08, 2013

    Bongo kula kwa TINDO!

    Nini miaka 7 iliyopita ulikuwa huku umesahau weweeee???

    Wajanja kibao walijifanya kuja Bongo kujaribu wameshindwa kurudi Majuu wamekwama huku.

    Endelea kula Mafao ya bure huko Norway, jaribu kurudi TZ oune cha moto utanasa!

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 08, 2013

    Kimoja tu ambacho kwa haraka haraka napenda kukukumbusha nikiwa kama mmoja wa waliobahatika kupata hiyo green card, ukienda ubalozini lazima watahitaji police clean report ya huko Norway na ya Tanzania. Kwa Tanzania unaweza ukaipata fasta ukienda pale Polisi makao makuu. Ila ya huko Norway jitahidi kuanza kuifuatilia sasa hivi ukiwa huko, otherwise watataka kuifatilia wao kupitia ubalozi wao wa Norway, sasa uombe Mungu hiyo ripoti iwe safi kweli, kwani wewe hutakiwi kuiona, hususan hiyo ya kutoka Norway, inatakiwa ikabidhiwe ikiwa sealed. Mimi niliwahi kuishi Uholanzi kidogo kwa mwaka mmoja, Ubalozi wakakomaa kutaka hiyo ripoti, wakahitaji niwape anuani kamili ya nilipokuwa nikiishi, wakafuatilia wenyewe Uholanzi. Ilichukua zaidi ya mwezi mchakato huo wa hiyo ripoti kukamilika.
    Jaribu kuangalia pia alternative ya kuomba kufanyia interview huko Norway ili usije ukakosa yote.

    Kila la kheri.

    Mdau Marekani.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 08, 2013

    Uliondoka Tanzania mwaka 2006 miaka 7 iliyopita kwa visa ya kubahatisha ya Norway.

    Kipindi unaondoka ulikuwa unauza Mitumba Mnadani.

    Sasa kwa taarifa yako ukirudi Bongo huwezi kuuza Mitumba tena wenzio wote sasa kuuaza Mitumba wameshapoteza,

    Mabosi wameweka watu wengine nako kwenye Mitumba kumejaa, wenzako wa kipindi kile hawana mchongo ni vile umewashit huwasiliani nao sasa wamebaki wanaosha magari.

    Wewe ukirudi Bongo utabeba zege.

    Shauri yako!

    ReplyDelete
  41. Kingo KisebengoMay 08, 2013

    Tafuta Lawyer wa immigration akushauri.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 08, 2013

    kalaga baho!

    wazungu wana akili sana, unajua dogo hawa watu wanawasiliana sana halafu ktk Mabunge yao wanashirikiana sana kuhusu kuwabana wahamiaji wanapoingia makwao.

    Ni vile lugha yao hujui, pia mengine wanajadili kwa siri ktk Kumbi za Serikali zao.

    Ktk hiyohiyo Norway pana jamaa yangu anaishi zaidi ya miaka 20 huko anaijua lugha Norwegian kinyume nyume aliwahi kusikia ktk Ukumbi mmoja wa Serikali jamaa Maafisa wa Juu wanabishana wakiwa ktk Kikao cha siri juu ya kuwabana Wageni!!!

    wameshawasiliana Marekani na Norway, sasa wamegeresha kukupa hiyo Green Card halafu wanakushauri urudi kuombea visa Bongo ili ukija bongo wakunyime halafu ujikute hata Norway kwenyewe utashindwa pia kurudi, UTAKOSA kotekote, utajikuta unabaki Tanzania.

    Hivi kazi ya Ubalozi wa Marekani huko Oslo-Norway ni ipi?, kwa nini wasikuache uombee huko huko?

    Wewe mtoto mdogo una rekodi gani ya uhalifu hadi kutakiwa uje uombee visa ya Marekani kwenu Tanzania?

    Nia yao wazungu ni wewe kurudi kwenu Africa wana mind sana sisi kwenda kwao lakini wao kuja kwetu ahhh visa wanachukulia Airport wanaingia kama kwao!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 08, 2013

    HUYU MDAU ALIELETA HII MADA KACHOMEKEA TU KUMSAIDIA AU KUWASAIDIA WATU AMBAO PENGINE WANAWEZA WAKAKUTANA NA MAZINGIRA YA NAMNA HII KIFUPI KAFANYA MCHEZO WA KUIGIZA

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 08, 2013

    Pole na hongera kaka
    Nakupa ushauri wa bure wala usirudi

    utachanganyikiwa bure kwa ile miaka saba na ukichanganya ya hapa

    umekataliwa kitakachobaki ni kunywa pombe na kuzungumza peke yako tu!
    Kaa huko huko kitaeleweka tu.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 08, 2013

    Kwanza hongera kwa ushindi. Pili gc zinatoka zaidi ya 50,000 na utoaji wake ni first come first serve.

    Lakini kwa nini unaogopa kurudi kwenu haswa bongo, ungekuwa msomali ingekuwaje? Tuache mawazo mgqndo ya mwaka sabini na mbili, kama huja make kwa miaka saba huko norway na bado unaogopa kurudi bongo bora usirudi, maana sio fighter wewe endelea na maisha yako uliyonayo. Kama ni fighter utakuwa katika position.nzuri ya kurudi bongo na kufuatilia gc yako na matokeo yoyote hayataathiri maisha yako. Bongo opportunity kibao. Nakwambia haya nikiwa nimeishi Norway na us vilevile.

    Kazi kwako na mawazo yako.

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 08, 2013

    Mkuu hongera kwa kushinda, wengine tulishinda ile ya 2012 kisha wakabadili matokeo mpaka leo sijashinda tena.

    Ushauri wangu ni huu;

    =>Kutegemea na case number yako ya DV notification letter, kama ipo karibu kuma matumani maana huwa wanachaguliwa 100k lakini viza zinatolewa kwa 50k tu kwa hiyo ni 50/50 chances zaidi ikitegemea utimizaji wa masharti na cas nambe yako. Hivyo

    # Jaribu kufuatilia uwezekano wa kutumia ubalozi wa marekani hapo Norway kufanya interview, japo uwezekano unakuwa mgumu haswa kutokana na hio ileggal status uliyonayo
    #Nenda bongo ukiwa na plan B za kurudi na kuanza maisha mapya, kuna fursa nyingi ukiwa na ujanja wa ulaya unaweza ukafanikiwa. Ikiwa watakunyima basi unajizatiti na kuendelea na maisha ya bongo maana najua kurudi Norway inaweza kuwa ngumu kidogo.

    Napenda kukushauri usikubali kushindwa jaribu kupata hiyo nafasi ya kuchaguliwa ni adimu mno weka nia ongea na wataalamu wa uzamiaji utaweza tu ndugu yangu.

    Kilalaheri

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 08, 2013

    Mwanangu usije ukachezea Bongo. Mbongo ana roho mbaya ya kuzaliwa akiona mwenziwe atafanikiwa. Pale kwenye balozi za Ughaibuni kuna Wabongo wameajiriwa kupokea maombi tu basi utafikiri wao ndio malaika wa kutoa roho. Njoo ungalie watu wanavyofanya kazi hapa kwenye balozi za Ughaibuni hapa UK utashangaa. Maana kabla maombi yako hayapokelewa wanahakikisha kila kilichohitajika kipo na kama hakipo wanakwambia pale pale ukarekebisha, mpaka maandishi kama umekosea wanakwambia. Sasa nenda Bongo uone hata akiona kitu umekisosea ndio atafurahia maana anajua utakosa tu. Mwanangu tafuta mwanamke uzae nae, hawakurejeshi ng'oo. AU uje Bongo ujue mbivu au mbichi!!

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 08, 2013

    Dogo nakushauri nenda kwenye ubalozi wa marekani hapo Norway ukamilishe masuala yako. Huna haja ya kurudi bongo. Hawawezi kukuuliza masweli mengi kama ungekuwa bongo zaidi ya kuwathibitishia kuwa wewe ndie uliyeshinda hiyo GC.Pia hawawezi kukuliza upo hapo kinamna gani.Peta njoo huku tule kuku.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 08, 2013

    Unataka kwenda Marekani ukafanye shughuli gani? Una uhakika na maisha ya Marekani kiasi ukaacha maisha yako ya Norway?
    Baki ulipo anzisha biashara uendelee na maisha.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 08, 2013

    Kijana Bongo ni JAMBALAND!

    Ukiwa huna ndio huna kabisa,

    Uliondoka mwaka 2006 Nauli za Madaladala Jijini Dar zikiwa Tsh. 150/= na sasa Nauli ni Tsh. 500/= hela ambayo kipindi kile ulipokuwa Bongo ulikuwa unatembea kwa miguu kwenda Mjini ukitokea kwenu Keko Toroli ili mchana utumie 500 yako kibindoni kwa mama ntilie kula Ugali na Maharage!

    Hivi sasa Ugali na Maharage kwa mamantilie ni Tsh. 3,500/= hela ambayo kipindi kile ilikuwa unakula Biriani kwa kuku!

    Dogo kwa kasi hiyo umeona uchumi jinsi ulivyoyumba?

    Je, ukirudi mapigo hayo kasi yake utaiweza?

    Kazi kwako, kusuka au kunyoa!

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 08, 2013

    Hongera sana kaka kwa kushinda hatua ya kwanza ya kupata green card.

    Kwa kifupi
    Interview stage huwa ni stage ya kuchuja wale waliodanganya hatua za awali, kwa hiyo hakikisha

    1. huwapi shaka kwenye your identity verification hii ni pamoja na majina yako yote tangua uzaliwe hata kama umebadilisha majina at one stage or another

    2. uweze kujieleza addresses zote ulizowahi kuishi, sikumbuki vizuri may be for past 10 years

    3. sehemu yoyote uliyowahi kuishi kwa miezi 6 au zaidi hata kama ni tanzania lazima uwe na report safi ya police

    4. uwape address moja ya utakaposhukia marekani...hii yaweza kuwa ya yeyote hata rafiki yako mradi naye awe marekani kihalali usije ukamuingiza matatizoni

    5. ufanye full medical test na vaccinations jinsi ulivyoelekezwa kwenye form pamoja na kulipia visa fees ... hii yote yaweza kukutoka kama $1,000+

    ni hayo tu kwa kifupi, kama yametulia....interview ni formality tu

    N.B: Unaweza soma maoni ya watu ila hakikisha unafuatilia na ukiweza kuprint any important information kutoka website ya state department, maana kuna wakati mwingine unaweza kukuta updates au kitu ambacho hujaambiwa lakini ni muhimu kisije kukuta kwenye interview date

    www.state.gov

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 08, 2013

    Dogo janja,

    Zinagtia tofauti ya maisha bongo (ingawa hujui kwa kuwa hukuwepo hapa), tofauti ya maisha Bongo tokea mwaka 2006 ulipo ondoka hadi leo hii mwaka 2013.

    UTAKUJA KUUKUBALI MSEMO HUU UTAKAPOTIA MAGUU BONGO NA KUKUTA UKISHUHUDIA MAMENO HAYO HAPO CHINI YA KUWA :

    ''things were fine during those good old days when Apple and Blackberry were fruits and not phones'' !!!

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 08, 2013

    Ohooo baki Norway.

    Rudi Bongo uone kama hukufyatua matofali!!!

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 08, 2013

    Utakuja kuwa Dakitari wa Upasuaji kwa kuwa Muuza Mafenesi!

    Maana mafenesi yamekaa kama tumbo la binaadamu na Muuzaji wake ni lazima ayapasue kwa kisu kama Dakitari anayefanya Upasuaji Hospitali!

    Utauweza huo Udakitari?

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 08, 2013

    Kaka vipi unaondoka Norway nchi tajiri unakimbilia Marekani? Aisee umefikiria vizuri kweli? Au labda kwa vile huna makaratasi ya Norway?
    Vile nijuavyo maisha ni mazuri sana Norway hata kushinda huko Marekani.
    Lakini nikuambie tu, pigana kiume upate unachotaka,hamna kinachoshindikana popote pale hata Bongo.

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 08, 2013

    Jamaa yangu naomba nikupe pole kwa maoni yote uliyopata. Kusema kweli watu wengi hawajui wanachoongea. Na ukweli hamna mtalaamu wala ilo. Kila mtu ana njia, nafsi yake, na bahati yake kufanya hayo mambo. Kwa wewe inabidi umpate mtu aliyepitia shida, na vipengele vile vile kama vyako kukujibu swali lako. Sasa humu jamaa wengi wanaongea upupuu tu, hata kama wamefika Marekani siyo kusema ndiyo wanajua jinsi ya kuingia na hiyo GC ya bahati. Siye Wabongo popote pale tulipo utalaam wetu ni mdomo, natunajua sana kupeta domo kuliko utalaamu na kama unavyoona hapa kwenye maoni. Halafu atuongei kwa kutia moyo bali kukatisha tamaa. Ndiyo maana wabongo tunakimbiana halafu jamaa wanaanza kusema jamaa analinga.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 08, 2013

    Hongera kwa kushinda, Swala lako nakushauri urudi Bongo ukiwa na Police report.Ubalozi wa Marekani hautajali ulikuwa na makaratasi ya kuishi Norway au la.Ukipata Police report usije ukaficha kuwa uliwahi kuomba kibali cha kuishi Norway kwani tayari jina lako liko kwenye EU central computers ambazo Marekani wana access nazo.Rudi kufuatilia bahati yako na ukukataliwa shukuru Mungu pia kwani kuzeeka Ulaya bila makaratasi ya kuishi huko ni BALAA tupu.

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 08, 2013

    ebwana kuhusu green card jaribu kuwa makini sana kwani marekani kuna argence nyigi sana za utaperi zipo wapigie sim american embassy waulize kama kweli umeshinda nakwambia hivyo mimi mwenyewe nilisha ingizwa mjini dalla kama 100 kwa family na baadae wakaniambia nimeshida hivyo inatakiwa nilipe pesa ya visa nikashangaa sana,badae nikamuliza mtu ambae yuko marecan akaniambia ukiwin green card hulipi anything do hapo nilipo shutuka hivyo jaribu kuwa makini.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 09, 2013

    Norway hapo hapo ulipo ni peponi!

    Nani kakwambia ya kuwa maisha ni lazima uwepo Marekani?

    Kinachokusumbua wewe ni mdogo na hujui kufuatilia masuala mbambali mbali yanayojiri ktk Dunia kila uchao.

    Hapo Marekani kwenyewe hali ya maisha inategemea na Jimbo unalikaa hali yake Kiuchumi ndio kigezo cha maisha kwa ujumla ni kuwa ukiwa ktk Majimbo tajiri maisha ni angalau MAZURI lakini ukiwa ktk Majimbo masikini maisha ni MABOVU afadhali ya Bongo, pana Majimbo mengi masikini maisha hayana tofauti na ya Bongo tena afadhali Bongo unaweza kulima matembele uchochoroni ukapunguza gharama za maisha.

    TOFAUTI YA MAISHA MAREKANI KULINGANA NA MAJIMBO NA HALI ZAKE KIUCHUMI:

    TAJIRI:
    -Washington DC
    -California
    -Texas
    -Washington Seattle
    -Oregon

    MASIKINI:
    -Kentuky
    -South Carolina
    -Arkansas
    -Alabama
    -Mississippi

    Hivyo ukienda Majimbo tajiri angalau una mwanzo mzuri na ukienda Majimbo hoi utajutia maamuzi yako kuondoka Norway!

    Zaidi ya mifano hiyo ya US:

    1.Niliwahi kumsikia jamaa mmoja aliehangaika sana na maisha akisafiri nchi za nje, mara anarudishwa akaja jaribu kwenda Msumbiji tena mji mmoja mbovu sana unaitwa NAMPULA huwezi amini jamaa alienda kutajirikia hapo na kutoka kimaisha kabisa akiwa ameweza kumilia Maelfu ya US$ Dollar za Marekani na Maelfu ya EURO !!!

    2.Hapa hapa Tanzania mnapo pakimbia ninyi ndugu zetu watu wenzenu humu humu wanatoka kimaisha kila uchao!, angalieni Wahindi na Wachina wanakuja kutajirikia hapa hapa Tanzania !!!

    NDIO MAANA WANASEMA MAISHA POPOTE LA MUHIMU MIPANGO YAKO NA MICHONGO YAKO!!!

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 09, 2013

    Shalom.

    Kaka nimesoma maoni ya wadau wote na kufikia itimisho la wewe endelea kubakia huko huko Norway kwa sababu zifuatazo:

    1. Kwanza ni vigumu kwa wewe kupata police report
    2. Umekaa nchi ya watu zaidi ya miaka 7 illegal so watakuambia wewe sio mwaminifu
    3. Kuna chance 2 kukosa hama kupata lakini asilimia ya kukosa visa ni kubwa
    4.Na ukikosa visa maana yake hauwezi kurudi tena Norway na japo Tz ni home lakini hakuna maisha hapa kaka to honest kaa huko huko tengeneza maisha
    5.Pia kuna kizingiti cha kuwa na mtu kule USA yan kama utafanikiwa watataka je utafikia wapi kule USA je una jamaa yoyote marekani? kama hauna basi kaka we tafuta maisha huko huko Norway chance itakuwa ndogo

    Ushauri wangu:

    1. Jaribu kuomba hiyo interview ifanyikie Norway
    2. Hata kama sisi tumekushauri vizuri namna gani najua tumeongozwa na roho wa bwana vile vile roho huyo huyo atayathibitisha haya kama utakaa kimya kumsikiliza. Leo usiku utakapo kwenda kulala omba Mungu akupe njia ya kufanya katika hili.

    Bwana hawe nawe na utafanikiwa yote kama utamweka Mungu mbele ya mambo yako yote.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 10, 2013

    Kwa nini usiombee hapo hapo kwenye ubalozi wa marekani??? Na kama hilo haliwezekani kwa sababu umekaa Norway kwa njia isiyo halali unadhani ukirudi bongo ndo utafanikiwa??? La hasha (unless kama wakati unaajiandikisha kwenye lottery ulisema uko Tanzania) Je, hii miaka saba uliyokaa Norway ulijaribu hata kujiendeleza kielimu?? Ni vizuri kuwa na plan B (kuwa incase ikitokea nikalipuliwa nirudi bongo niwe na pa kuanzia na elimu ambayo nimejikusanyia nikiwa ughaibuni). Nasema hivyo sababu ikitokea ukarudi bongo na usifanikiwe, Tanzania ya sasa bila elimu na mawazo ya maendeleo ni ngumu sana....fikiri tofauti, chukua hatua

    ReplyDelete
  62. hongela sana hata kwa kuishi uko Norway!nivyema sana ninafulahi watanzania tuna respond positively kwa ndugu zetu wanao omba ushauri! basi nivizuri tusaidiane maana maisha ni popote na dunia ni ya Mungu wetu aliye juu, swala ni kwamba mtu huzaliwa sehemu fulani lakini tunaweza kuchagua kuishi sehemu zingine sio vibaya!kwakweli bongo life linabana mpaka mwisho,mambo ni magumu hapa! mimi naomba ninapenda kuishi USA,kama kunandugu yupo anaweza kujitolea kunisadia na nifanye mchakato wa visa USA,tusaidiane aisee,tuvutane nasisi tutoke huku!tusaidiane ndugu zangu watanzania,email gwamakamwakyambiki3@gmail.com

    ReplyDelete
  63. Naomba kujua namna ya kuandika green card

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...