Hii picha imenifanya nijiulize maswali mengi... wewe je? (ongeza kwenye comment)
1. Hayo maandishi yaliyoandikwa nyuma ya gari hilo ni wangapi wameweza kusoma? (OANGEZ, DANGEZ...)
2. Tanzania tunatumia lugha ya kiswahili zaidi, na kwenye gari hilo la mafuta hakuna neno lolote la kiswahili kumjulisha mtanzania kuwa hilo gari limebeba nini? na usalama wake ni nini?
3. Hapo inaonyesha hilo gari inamwaga mafuta kwenye tanki la chini la kituo cha mafuta katikati ya jiji la Dar es Salaam, na hakuna mhudumu yoyote aliyopo jirani nayo. je ikitokea bahati mbaya nani wa kulaumu?
4. Ndoo moja imelala chali jirani na kisima hicho... ilikuwa na nini? Maji/Mafuta/Mchanga...
5. Usalama wa gari na mali uko wapi?
6. Nijuavyo mimi, kila gari la mafuta inapewa sticker fulani ya kujulisha kuwa hilo gari limebeba mafuta ya aina gani, na kwenye ajali litazimwa na aina gani ya zima moto? kwenye gari hilo iko wapi?
7. Hiyo alama iliyoandikwa kulia la gari hilo (juu ya reflector) lina maana gani?
8. OSHA / EWURA / FAYA / N.K. ... mpo?
Hapo panasomeka danger sema nadhani imekuchanganya herufi (r)ya mcharazo tu.
ReplyDeleteNa maandashi ya wafadhili chini kulia hukuyaona.....ni kichina maana yake ni danger....
ReplyDeleteNdio maana nimejifunza lugha yao...
Ni ww tuu labda mtupu kichwani hilo ni neno linaonekana kabisa ni DANGER bila hata kuuliza ungejua mapema hilo tanker la mafuta...na bongo lugha zetu kuu ni mbili english au swahili how come usome OENGEZ???
ReplyDeleteToo conscious..!! Chapa kazi wewe acha longolongo..Muda uliotumia hapa ungeutumia kujenga maisha yako na Taifa lako.Acha porojo.
ReplyDeleteMdau ameleta mada yenye mantiki sana, lakini wadau hawauoni umuhimu wake. Ajali ikitokea wadau hawa hawa wataanza kuilaumu serikali. Ingawa kabla ya ajali hawayaoni makosa ya utendaji.
ReplyDeleteHuyu mleta mada ana pointi muhimu sana,ni bahati mbaya hakueleweka vizuri kwe wengi.Maandishi ya tahadhari yanatakiwa yasomeke vizuri na yaeleweke haraka.Sehemu nyingi maandishi ya tahadhari na hayatumii ITALIC na mbwembe zingine.Tumesahau kwamba kuna watu wana matatizo ya macho.Siyo kwamba kila mmoja anaweza kusoma hayo maandishi kiurahisi.Proactive>reactive....
ReplyDeleteduh?? tumeingiliwa na wachina.
ReplyDeletetujenge Taifa bila Usalama?
tungoje maafa ili tujirekebishe?
jamaani sio hilo gari tu kwa usalama pengine hata drive mwenye hana driving licence
ReplyDeleteWACHANGIAJI NAONA MMECHANGIA POINT MOJA TU AMBAYO HAINA MANTIKI YOYOTE YAANI NENO DANGER....JE KUHUSU HIZO STICKER NYINGINE KUONYESHA NI MAFUTA GANI YAMEBEBWA N.K...KIUFUPI GARI HALIJAONYESHA UTAHADHARI WOWOTE HATA BAJAJ MTU ANAWEZA ANDIKA DANGER....DANGER PEKE YAKE HAITOSHI....WENGI WENU HAMJAWAHI ISHI NJE YA NCHI NDO MANA HAMJAONA JAMBO HATA MOJA LA KUSHANGAZA KATIKA HIYO GARI...WALOWAHI KUISHI NCHI ZILIZOENDELA UTAPATA KASORO NYINGI KATIKA HILO ZOEZI NA GARI YENYEWE.
ReplyDeletechuki zako binafsi kaka hizo inasomeka hiyo mwake...
ReplyDeleteHapo ni garage na gari hilo ndiyo linaandaliwa kwa kazi labda ya kubeba mafuta. Hicho ni kisima cha maji. Kabla halijabadilishiwa kazi lilikuwa linabeba maji!
ReplyDelete