Mashabiki wa Yanga, Kuendelea kurekodi matukio ya furaha Jumamosi??
Mashabiki wa Simba.....wataendeleza Kidedea hiyo siku ya Jumamosi???
Tiketi kwa ajili ya pambano la kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba na Yanga,zitakazokutana kesho (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar zinaanza kuuzwa leo (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali vya jijini Dar.
Vituo vitaanza kuuza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni na vitakuwa kama ifuatavyo,ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.
Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A.
YANGA UGOLO YANGA UGOLO, SIMBA IMARA SIMBA IMARA.
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Yanga Ugolo?
ReplyDeleteHadi sasa Kombe lipo makwapani kwa nani kwa Yanga au Simba?
Wewe ndio walewale wakati wa Kupigana wau wawili unakuta unapigwa unapiga kelele mshikeni nitamuuwa wakati wewe mdiye uliyechini unanyukwa!
Mtoa Maoni wa kwanza juu:
ReplyDeleteMshindi Yanga hana kelele, tayari Kombe lipo kibindoni.
Tunachosubiri kilichobakia ili TUMALIZIE VIZURI sisi Yanga S.C siku hiyo ni kulizamisha kwa mara ya pili tena LIBOLO !
yanga kabong`oa Simba ........
ReplyDeletewote nyie hamna akili mnashsbikia mipira badala ya kazi,shabikieni kazi nchi isonge mbele!
ReplyDeleteushauri kama mtu hana mshipa ukiamabatana na kitambi basi asikubaliwe kuwa mwanachama wa yanga,na kama amesoma sana basi ni vema akajiunge na klabu ya msimbazi sisi mwisho darasa la saba.
ReplyDeletehakuna kulazimishana hii ni demokrasia na uhuru wa kujiamulia kiutawala.
asante.
mdau.
kaliakoo,daleslamu.
Mdau wa wa juu wa Msimbazi:
ReplyDelete''yanga kabong`oa Simba ........''
Wewe ulitufunga Yanga Mabao 5-0, kwa Mashuti ya miguu na Vichwa.
Sasa wewe Simba ukafungwa Mabao 5-0 afadhali jamaa WANGETUMIA HATA MABAO YA MIKONO KAMA MARADONA wao jamaa WAKAWAFUNGA SIMBA wakitumi LIBOLO!