Benki ya NMB imeendelea kuwa karibu zaidi na jamii inayoizunguka kwa kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii hususani katika sekta ya elimu. Kama ilivyo ada kwa benki ya NMB hutoa sehemu ya faida yake ili kuisaidia jamii. Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati yenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa ajili ya shule ya msingi Mangapwani na Bumbwini mjini Zanzibar.
Meneja Masoko wa Benki ya NMB, Shilla Senkoro akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10/- mke wa makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Mama Asha Balozi madawati yaliyotolewa na benki ya NMB.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bumbwini na Mangapwani wakiwa wamekaa kwenye madawati waliyoyapokea kutoka Benki ya NMB kama msaada ili kupunguza uhaba wa madawati unaozikabili shule nyingi nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...