Rais wa Marekani,Mh. Barack Obama.

Kuanzia tarehe 26 Juni hadi 3 Julai, Rais Obama na Mkewe wanatarajia kutembelea nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. 

Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa. 

Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla.

TAARIFA TOKA WHITE HOUSE, MAREKANI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2013

    Mdau anony hapo juu mtaje tu ni William Malecela kuwa kaleta habariza uongo kuwa Kingunge Ngombare Mwiru hatunaye. Huyu jamaa ana matatizo ya inferiority complex. Hata ndugu zake nasikia haelewani nao. Maisha yamemshinda Marekani sasa kaja Tanzania kutuharibia mambo. Wadau Mwgopeni huyu mtu kama ukoma!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2013

    Hehehe, Obama anakuja naona barabara zitapigwa deki

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2013

    Sijui mtaa gani utabadilishwa jina na kupewa jina lake? au sijui atapewa kiwanja kigamboni? au daraja la Kawe ,mlalakua litapewa jina lake?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2013

    Woiyeeeeee! Kichwa kinakuja kukazia Utandawazi/wizi. Na uwana Sesere wetu tumekwisha

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 22, 2013

    It is not kuja kuwasalimia tu. Huyo huenda mahali ambapo pana possilbe au kuna American interests. You have uranium. George Bush alitua bongo, hakuna cha ajabu.

    ReplyDelete
  6. Tehe, tehe, tehe, Watanzania tumekwisha. Hawa mabepari sio size yetu na Hayati Mwalimu Nyerere alisema "MKINIONYESHA HUYO MJOMBA NITACHEKAAAAAA"
    Tumuombe Mungu hawa hawako kwa maslahi ya watanzania. Dunia ni kubwa.tehe, tehe, tehe, teheee!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 22, 2013

    jamani! tusiwe na chuki na roho mbaya, mgeni anakuja kwako unawaza anakuja kukuibia, tuamke tujijenge sio kujisononesha, mbona mnaenda kwake kila mara! tumejazana wa tz ibao USA!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 22, 2013

    Nafikiri tusiwe wakosowaji wa kila jambo na tusiwe tunaona kila jambo kwa negative attitude.. Ujio wake unafaida sana na of course hamna uwekezaji usiokuwa na bilateral benefit.. Kuna maendeleo makubwa tu ya mahusiano na nchi kubwa kama hii na wapo wengi wanaoutaka uhusiano huu.. Tuwaamini viongozi wetu tuliowachagua na pale wanapokosea tuwawajibishe

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 22, 2013

    AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAKWISHNEI

    ReplyDelete
  10. huyu anakuja kutembea tu kwa vile ana asili ya Ki Africa sera ya Marekani zamani kusaidia Africa ni mambo ya ukimwi hakuna chengine.

    Mi nataka aje hasa atembelee na Zanzibar kule tena hiyo tarehe moja anokuja kuna bongo la mkutano daaahh

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 22, 2013

    ANAKARIBISHWA KWA MIKONO YOTE ,KARIBU OBAMA NA NAMUOMBA AKAHUTUBIE BUNGE LA KITANZANI LA WALA RUSHWA WAJIFUNZE DEMOKRASIA MAANA YAKE NINI KARIBU SANA, KENYA MTAJIJU!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 22, 2013

    Mimi naona akifika tu ,ule mtaa wa mbezi beach kuanzia Kawe keepleft baada ya Mwai kibaki iwe Jina Lake BARAKA OBAMA AVENUE, mpaka roundabout nyingine kwa Joseph Kusaga. Kwani huo ndio mtaa iliofanana na mindhali ya Marekani,

    Na ule mtaa kutoka kona ya Africana kwenda white sand uwe WASHINGTON BOULEVARD. Hayo ni maoni yangu kwani naona tunakwenda tu kila siku marekani kama ndio MACCA yetu kwani kila mtu anaongelea huko tu ndio kama ibada yetu ya hivi sasa kwa hiyo naona tujipe moja kwa moja !

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 22, 2013

    Tunakukaribisha sana nyumbani raisi Obama. Wewe ni shujaa, nasi watanzania tunapenda mashujaa, haijalishi policy zako zinapendwa huko Marekani au la, wote walio pita kabla yako walipendwa kwa mengine na kuchukiwa kwa mengine, Hata huku TZ viongozi wetu tuna wa treat hivyo hivyo, so karibu suijali, ulibadilisha historia ya watu wenye damu ya kiafrica marekani, sahizi dunia inatutazama kwa mtazamo mpya hahaaa.

    Ila kweli wazungu wanatisha, kwa unafiki tu hawajambo, huku ughaibuni nawatazama siwamalizi, wanakupenda wakijua kuna jambo watapata toka kwako, wezi wa idea ile mbaya, kwa kujitajirisha kupitia migongo ya wenzao (wanjonge) hawajaanza leo. Ila viongozi wetu wawe makini hakuna ku sign mikataba isiyoelewaka, wasikubali kushurutishwa, kama vipi tuache madini yetu yalale huko aridhini ikifika wakati vizazi vijavyo vikawa na uwezo wa kuyachimba na kunufaisha taifa, basi itakuwa vyema. Ni heri yabaki aridhini kuliko tuibiwe, ya toke kwetu, yachibwe na wana nchi wetu bila vifaa vya kujikinga waishie kupata saratani huko baadae, kufaidi wafaidi wengine, hizo nyakati zilisha pitwa na wakati sahizi tuko macho kweli kweli, kama unabisha uliza mtwara.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 22, 2013

    Kweli kabisa mgeni anakuja mkaribisheni kwanza kabla hamjamuhukumu..Karibu Obama kwetu Tanzania ukutane na ufisadi,wizi,uchochezi,uchonganishi na maugomvi yasiyo ya maana ya kidini

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2013

    MTU MWEUSI HATAJIFUNZA HATA SIKU MOJA. HATA AKISAFIRI BADO USINGIZI WAKE NI MZITO SANA. SAMAHANI MICHUZI MIMI NASEMA WANA KHERI WALIOUKOSA UGENI HUU.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2013

    mama weeeeeeeeeeeeeee madini yetu jamani ndio yanafuatwa sisi tutabaki maskini mpaka lini????????????????.Michuzi ugeni huu una walakini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...