JESHI la Polisi Mkoani Morogoro limefanya msako mkali katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na wilaya ngingine za Mkoa huo na kufanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 33 wakituhumiwa kufanya makosa ya uhalifu na utengenezaji wa pombe haramu ya gongo na usafisishaji wa bangi.

Askari Polisi wakiongozwa na Makamada kuanzia mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, walifanya msako huo walianzisha msako huo katika maeneo ya Kata ya Lukobe, Kingolwira na maeneo mengine na kufanikiwa kukamata pombe haramu ya gongo lita 600, mitambo 22 , vyombo vya kupikia 124 , madumu 60 na magunia manene ya bangi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongike , alisema hayo Mei 22, mwaka huu alipozungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake na kuwaonesha vitu hiyo vilivyowekewa eneo la viwanja vya Ofisi ya Polisi Mkoa.

Hata hivyo alisema katika opareshani hiyo , Polisi imefanikisha kukamatwa kwa meno vipande 320 vya Kiboko na meingine mawili ya Nyati katika Wilaya ya Kilombero.

Katika hatua nyingine Polisi imefanikiwa kumtia mbaroni askari wa zamani mwenye cheo cha Koplo Usu Omari Abdallah ambaye alifukuzwa a uaskari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) Kikosi cha Ruvu, Mkoani Pwani baada ya kukutwa akiwa na sare ya Jeshi hilo.

Hatua ya kukamatwa kwake ilitokana na taarifa ya raima mwema na kwamba mtuhumwa alikuwa akiishi eneo la Msamvu , Manispaa ya Morogoro

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, askari hiyo wa zamani wa JWTZ licha ya kufukuzwa kazi aliendelea kubaki na sare za Jeshi hilo ‘ combati’ kinyume na sheria za Majeshi na kuitumia katika kufanya uharifu wa kutampeli wananchi.

Hata hivyo Kamaanda huyo wa Mkoa , alisema Opereshani hiyo ni endelevu na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kutokomeza mambo hayo ya kiharifu mkoani Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile ( mwenye fimbo) akiangalia mifuko ya mbolea iliyobadirishwa kwa baadhi kuwekwa mbolea Minjingu katika mifuko ya mbolea yenye nembo ya aina ya CAN baada ya kuikamata hivi karibuni katika ghala la mfanyabiashara wa Duka la Pembejeo za kilimo eneo la Nane Nane , Mjini Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile akiwaonesha Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) baadhi ya vitu vya aina mbalimbali ikiwemo mitambo ya kupinga pombe haramu ya gongo, mapipa , madumu na mifuko ya mbolea iliyochakachuliwa, viroba vya bangi na sare moja ya JWTZ ,ambayo kwa pamoja vilikamatwa na Polisi wakati wa oparesheni iliyioanza Mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, mwaka huu mkoani Morogoro.
Baadhi ya Askaari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro walioshiriki oparesheni ya ukamataji wa mitambo na mapipa ya gongo.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    IYAAAA! Sasa Gongo itapanda bei, loh!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    kuhusu nyara za serikali na uniform za kijeshi,hakuna mjadala.bangi kunauwezekano siku za usoni ikajadiliwa na kuhalalishwa, maana yaweza kuwa dawa ya magonjwa sugu.lakini gongo intakiwa kujadiliwa sasa hivi,ni kinywaji kinachohitaji kua DILUTED siajabu kidogo tu, kisha kuhalalishwa na kuanza kuwaingizia wazalishaji kipato kizuri, hata inje ya nchi kinaweza kuuzwa.Ndugu zangu wa kemia tupieni jicho hapo mnaweza kupata nishati ya kuendeshea mitambo, ikawa invention hio. ndio ajira hizo mnaweza kuziunda na kuwafanya vijana wakawa na pub zinazo leta kodi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Kazi nzuri mmefanya. Lakini zuieni na biashara ya pembe basi!Mbalance kotekote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    Sasa watu hawa ambao hawana uwezo wa kununua bia wanye nini? Kwanini kila kitu kisichokuwa cha kizungu mnakiita haramu? Kama gongo ni pombe haramu, kwanini bia siyo pombe haramu?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2013

    Hivi vitu vidogo vidogo ndivyo vinakamatwa. Lakini wasafirishaji pembe za ndovu, wasafirishaji wa wanyama hai, wahamishaji wa fedha kwenda nje ya nchi kiharamu , hao hawaguswi. basi watengeneza gongo na wauzaji achana na kazi hizo. anza kusafirisha pembe za ndovu na fedha na wanyama hamtakamatwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2013

    Hiyo USA inaitwa "MOONSHINE" mpaka marais wamekunywa huko!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2013

    very strange, whats wrong with gongo? vigogo wanakula nchi lakini hawashikiki. Hawa wadogo mnaoshika, wanatafuta mlo daily. Shame on these police.

    ReplyDelete
  8. manka-mzaMay 23, 2013

    waacheni watu wafanye bness zao, kikubwa walipe kodi waingizie serikali kipato.inaonyesha hiyo ni pombe km pombe nyingine tena ina wateja wengi.nyie wenyewe polisi ni wateja wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...