Na Abdulaziz Video
IMEELEZWA kwamba zaidi ya watoto 15444 wanaoishi katika mazingira
magumu na hatarishi mkoani Lindi wametambuliwa na wameanza kupatiwa
huduma muhimu za kijamii kwa lengo la kuboresha maisha yao kupitia
mradi wa pamoja tuwalee.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa uwezeshaji uchumi kwa familia
zinazoishi katika mazingira hatarishi mkoani Lindi kupitia shirika la
PACT Tanzania,Rehema Madusa kwenye hafla fupi ya kukabidhi baskeli
kumi na pikipiki moja kwa ajili ya wawezeshaji wa watoto hao
wanaoishi kwenye mazingira hatarishi katika kata kumi za wilaya ya
kilwa.
‘watoto hao waliotambuliwa wanalelewa na walezi 2617 wakiwemo
wanaume 480 na wanawake 2137 kutoka vikundi 192 vilivyo undwa kutokana
na familia duni za watoto hao kutoka kila wilaya
Kwa mujiu wa mratibu huyo mpango huo wa pamoja tuwalee wa miaka
mitano ulianza kutekelezwa mwaka 2010 ukiwa na malengo saba kwenye
maeneo ya elimu,afya na lishe, ulinzi wa watoto, msaada wa
kisaikolojia,msaada wa kisheria, hifadhi ya jamii, na huduma ya
kuboresha kipato.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...