Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA. Bi Jayne Nyimbo akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF alipotembelea banda la PPF lililopo viwanja vya Mw. Nyerere Dodoma inapofanyika wiki ya Hifadhi ya Jamii. Kulia ni Meneja Uhusiano wa PPF Bi. Lulu Mengele akimpa maelezo ya jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na Mfuko Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya SSRA Ndg. Kabeho Solo.
Mhasibu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Grace Fihavango akipokea mchango kutoka kwa mwanachama mpya, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA. Bi Jayne Nyimbo mara baada ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF alipotembelea banda la PPF katika wiki ya Hifadhi ya Jamii yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere Dodoma. Wanaoshuhudia kutoka Kushoto ni wajumbe wa Bodi ya SSRA Bw. Juma Muhimbi na Bw. Kabeho Solo pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi. Sara Kibonde Msika.
Mbunge wa Busega (CCM) Mh. Dr.Titus Kamani akipata maelezo kuhusu Mafao na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Afisa wa PPF Bi. Maurecia Mbena alipotembelea banda la PPF kwenye viwanja vya Nyerere Square Dodoma inapofanyika wiki ya Hifadhi ya Jamii.
Mfuko wa PPF unawakaribisha wananchi wote kutembelea kwenye banda la PPF ili waweze kupata elimu ya mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...