Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro. Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

Bw. Wilson M. K. Masilingi (kulia) Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora. 
Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga (kushoto) , ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

Bw. Modest Jonathan Mero (kulia), ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva. Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang’ka Marmo  (kushoto) kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.




John M. Haule
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 
DAR ES SALAAM.
12 MEI, 2013



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2013

    Hatimae uholanzi sasa tumepata balozi wetu maana safari za kumfata balozi ubeligiji zilikuwa za shida sana

    Asante sana mheshimiwa rais kwa uteuzi wako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2013

    HERI YENU MLIECHAGULIWA KUWA MABALOZI MMELAMBA DUME LA NGUVU SANAA.MDAU MBEBA BOX LONDON.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2013

    Mbona Mh.Dkt Jakaya umesahau hapa kwetu Russia kutuletea Balozi mpya? Tunasubili kwa hamu kujuwa nani atakuja huku maana Russia na nchi zinazokuwa chini ya Balozi huyo ni muhimu sana. Tuletee Mh, anayejuwa kuongea na kushawishi wawekezaji na awe mtu anayeweza kutembelea maeneo yake yote na kushawishi wafanya biashara kuja huko kuwekeza na pia kutangaza Utalii wetu kwa nguvu kwa kuwa nchi hizi ndo zenye watumiaji ikija kwenye mambo ya Utalii. Mtalii mmoja toka nchi hizi ni sawa na watalii 30 toka Uingereza wanaokuja hapo nikimaanisha pesa atakazotumia akiwa hapo nchini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2013

    Mhe.Sang'aka Marmo anaperekwa kwenye uwanja wa FFU ughaibuni akina ras makunja wa virungu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2013

    There was an embassy when I studiied in the Hague. I think they closed and now re-opening it. It costs money to run those things. Is Brussels really far? even Paris is not far at all.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2013

    Kikwete, Mheshimiwa! hakuna jinsia nyingine inayokwalifai baba?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2013

    Hongera kwa kufungua ubalozi uholanzi kwani kutufungua fursa nyingi za kiuchumi ila na swali moja tu kwa wakubwa.Hivi Wizara ya mambo ya nje pale hakuna Watanzania waliofikia hadhi ya ubalozi wapewe hizi nafasi ?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2013

    Hongera sana kwa uteuzi Mkaitangaze Tanzania vema kwa rasilimali tulizonazo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2013

    Hongereni wateuliwa nyote, ila muende huko kikazi na kitaifa kwa ujumla. Majungu,anasa na ubinafsi iwe mwiko kwenu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2013

    wazanzibari hawamo!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2013

    Wewe Mzanzibari wa 10 (kumi) Wazanzibari waliobaki na wengineo Wabara watakwenda kuvua Samaki na kushiriki Kilimo.

    Haiwezekani Kila Mtanzania Bara na Visiwani (KAMA WEWE NA MIMI) apate kazi ya Ubalozi ama Serikalini!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2013

    Nini Mzanzibari wa 10 juu hapo.

    Ninyi mpo watu wawili (2)tu nchi nzima halafu kila mmoja apewe kazi nani atapika urojo na kukaanga mihogo?

    Je, sisi akina Maganga Bara ambao tupo mamilioni tuseme nini?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2013

    hahahahaha!

    Makame ndugu yangu kama hujateuliwa kuwa Balozi ya nini tabu kung'ang'ania kukaa Kisiwani?

    Isiwe tabu wewe panda Boti uje huku Bara kwa mimi nduguyo Maganga ili tuhague moja kati ya:

    1.Tuakasome ili na sisi tuweze kuteuliwa ktk Ubalozi!

    2.Nchi yetu JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ni kubwa saana!, hadi kwetu huko Kwimba na Malampaka Shinyanga ukija Kijijini watatupatia Ekari kadhaa na tutafungua Mradi wa Kilimo kwa Mkopo kutoka tawi la Chama Chetu CCM hapo Kijijini!

    3.Kama hutaweza kushiriki Kilimo kama mimi mwenzio Maganga wa Bara ambaye ninalima kama Trekta, tutakwenda Mbozi ama Maganzo kununua na kuuza Dhahabu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...