Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila akizungumza na wananchi wa Mji wa Lindi wakati upokeaji Tuzo za Bia ya Safari Lager mkoani kwake jana ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilikuwa Mkoani Mbeya. Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila (katikati) akiwa ameinyanyua tuzo ya Ubingwa wa Jumla ya Tuzo za Bia Bora Afrika ambayo Bia ya Safari Leger inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi mjini, Dk. Hamid Nassor (kushoto) na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mji ni Dk. Hamid Nassoro wakiwa ameshikilia tuzo ya Ubingwa wa Jumla ya Tuzo za Bia Bora Afrika ambayo Bia ya Safari Leger inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wengine katika picha ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Mwakilishi wa TBL mikoa ya Lindi na Mtwara, Bariki Massawe.

Wakazi wa Mji wa Lindi wakiwa na furaha na tuzo za Bia ya Safari Lager wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia ya Safari Lager ambapo jana walikuwa Mkoani Lindi.
Kwanini watendaji wa serikali wapige debe ushindi wa TBL kiasi hiki, Serikali inabidi kufocus kwenye dhiki zinazo wakabili wananchi ili kuwakwamua na shida za maisha. serikali ipromoti michezo na sanaa kwa vijana na kuwasaidi kuacha vijiwe na kuwa wabunifu wa kazi binafsi. kupromoti Bia kiasi hiki kuna faida chache za kiuchumi lakini madhara yake ni makubwa, bia ni starehe, serikali isijitie kimbelembele wacha TBL wafanye matangazo yao wenyewe na watakao kubaliana nao watakunjwa bia zao. ila si kazi ya serikali kuwashawishi watu kua TBL wanapika bia nzuri so kunywa Bia ya TBL. Mataifa yaliyoendelea yana sheria kali za pombe na huwezi mkuta mtendaji wa serikali akiinadi Pombe.
ReplyDelete