Waendesha mada katika semina ya kuangalia changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki na njia za kuzitatua wakijadili umuhimu wa elimu ya muziki katika soko la muziki, kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Action Music Tanzania, Mandoli Kahindi, Mkurugenzi wa sanaa kutoka Global Music Academy Ujerumani,William Ramsay, Muaandaaji wa muziki wa Uganda, Kazi Kasozi na Mkurugenzi Mtendaji wa Ketebul Music Kenya, Tabu Osusa
Semina hiyo ambayo inaambatana na maonyesho ya kazi mbalimbali za muziki yameandaliwa na Bayimba Cultural Foundation ya Uganda ambapo wadau mbalimbali wa muziki kutoka nchi mbalimbali wamejumuika kujadili na kubadilishana uzeofu juu ya soko la muziki kwa nchi za Afrika Mashariki. picha za matukio zaidi tembelea DOADOA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...