MAREHEMU WILLIAM VEDASTUS MUGURUSI
(1943 – 2013) 
Familia ya Marehemu, Bwana William Vedastus Mugurusi wa Kijitonyama Dar es Salaam, inapenda kutoa shukurani zake za dhati kwa wale wote walioshiriki nao katika kumuuguza na hatimaye kifo cha mume, baba, kaka na babu yao mpendwa kilichotokea siku ya Jumanne tarehe 16.04.2013 katika hospitali  ya AMI Wellness Center na kuzikwa Ijumaa tarehe 19.04.2013 katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.
Shukurani za pekee ziwaendee madaktari wote na wauguzi wa hospitali za Apollo,(India) Aga Khan na Ami Wellness Center ambao walijaribu kwa kadri ya uwezo wao kuokoa maisha ya mpendwa wetu; Uongozi na timu nzima ya Globe Accountancy Service (GAS) kwa ushirikianao wao wa hali na mali; Mapadri na wahudumu wote wa Kanisa Katoliki kwa huduma za kiroho; AAR, FHI360, ndugu, jamaa, marafiki, wanajumuiya ya Mt. Damiano Mfia Dini, na majirani wote.
Kutokana na ukweli kwamba siyo rahisi kumshukuru kila mmoja kwa jina, tunapenda kuwahakikishia kwamba tunathamini ushiriki wa kila mmoja kwa njia ya pekee, ushiriki ambao umeendelea  kutupa faraja wakati wa kipindi hiki kigumu. Tunawasihi tafadhali kila mmoja apokee shukrani zetu za dhati katika uzito ule ule.

Kutakuwa na misa ya shukrani tarehe 25 May 2013, saa 4 asubuhi nyumbani kwa marehemu William Vedastus Mugurusi, Kijitonyama.  WOTE MNAKARIBISHWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...