Familia ya Marehemu Acp (rtd) Bruno Damiani Matembo wa Ukonga, Dar es salaam, inatoa shukurani kwa wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha msiba wa Baba yao Mpendwa Mzee Matembo (pichani) ambaye alilazwa katika nyumba yake ya milele Ukonga, jijini Dar es salaam.
Shukurani ziwafikie Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Viongozi wa dini walioongoza Misa ya kumuombea Marehemu, Madaktari na Wauguzi waliojitahidi kuokoa maisha ya Mzee Matembo, Majirani na wana Ukonga
Tutaendelea kukumbuka daima Baba yetu Mpendwa kwa kwamalezi bora uliyo kuwa umetupatia hatutakuangusha kamwe kwani hata wajukuu wako wameyafuata maelekezo yako uliyo kuwa una wapa yakuwa nanidhamu kwa watu Wote Kuipeda Nchi yetu na Kutii Serekali pamoja na Mamlaka zake
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA
JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMEN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...