Mtanzania na Mkenya waliingia supermarket moja jijini London, walipotoka Mkenya akawa anajigamba kwamba wakenya ni wajanja kuliko wa Tz huku
akimwonyesha mTz chocolate 3
alizoiba supermarket, mTz
akamshawishi warudi tena ili na yeye akamwonyeshe ustadi wake.
walipofika ndani MTz akamwambia
mhudumu nataka nikuoneshe
mazingaombwe, hebu niletee
chocolate tatu, yule mhudumu
akazileta, jamaa akazila zote
mbele ya mhudumu halafu akasema
unaona nimekula chocolate tatu
lakini amini usiamini chocolate zako
zote zipo mfukoni kwa huyu jamaa,
mhudumu akamkagua Mkenya
mfukoni akachukua chocolate zake
zote 3 huku Mkenya akabaki ameduwaa.
je, nani mjanja kati yao??
Mtanzania na Mkenya madereva pale London kwa bahati mbaya wakagongana,magari yao yakaharibika ile mbaya,lakini wao wakatoka kwenye accident hiyo salama kabisa.Ndani ya gari ya mtanzania kulikuwa na chupa ya champeni ambayo haikuvunjika,akaifungua na kumpa glasi mkenya, cheers.Baada ya dakika hivi mkenya akamuuliza mtanzania, mbona wewe hunywi?Akajibiwa, nitakunywa, lakini kwanza nangojea traffic wafike.(Samahani original joke)
ReplyDeleteHAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAA
ReplyDeletewote wezi hakuna mjanja; mtaenda kujibia.
ReplyDeleteInabidi ule unachotolea jasho ndiyo ujanja; nje ya hapo si ujanja.
Kwa hiyo hakuna mjanja kati yenu ninyi; yani si mtz wala mkenya;
wote mukajifunze kutoa jasho kupata hitajio na si vinginevyo.
Hakuna mjanja hapo, mmoja mwizi na mwingine anaona noma kupelekana polisi!
ReplyDeleteMtz funiko!
ReplyDeletePana sehemu kama Burundi Mtz hapandishwi Kizimbani Mahakamani kwa kuwa anajua sana kujieleza ni lazima atashinda Kesi.
Si mchezo wizi ni Kipaji!!!
ReplyDeleteIngine ya ujanja wa aina yake,
ReplyDeleteMsomali mmoja alikuwa Mpakani Namanga lakini upande wa Tanzania, akawa na Lori na Tela lake.
Lori lilikuwa na namba za usajili za Tanzania, wakati Tela lilikuwa na namba za usajili za Kenya.
Msomali akapigiwa simu ya kuwa afunge Tela aendeshe kwenda Arusha, kwakuwa Tela la Lori lake lipo huko na Kichwa cha Tela la Kenya kipo Arusha.
Ile Msomali anaingia mjini Arusha akasimamishwa na Trafiki akaulizwa je inakuwa Lori ni la TZ na TELA la Kenya uedneshe?
Msomali akajibu ''Shio aajabu Kichwa Tansania nakaribisha kutembesha Mkia Kenya''
akisema KICHWA CHA TANZANIA KINAUKARIBISHA KUUTEMBEZA MKIA WA KENYA!!!
Mtanzania mjanja mana mkenya hawezi kwenda kushtaki popote kwa kuwa hakuzilipia chocolate na zimerudi tena dukani! Akili ni nywele kila mtu ana zake.
ReplyDeleteHm. Aliyesema wizi ni kipaji noma!!!
ReplyDeleteIla watanzania ulimwengu mzima wanasifika kwa wizi na utapeli ila siyo wajanja. maana wanaiba na wanakamatwa. Ila kuna badhi ya maeneo kwenye inchi jirani ambako watanzania ikifika mida ya jioni hawasogelewi kwa kusemekana hawaachi kitu,