Taasisi ya kuhamasisha maendeleo na mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara yaJAMII INFORMATION NETWORK inatarajia kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha  Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasishaMaendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano ndani ya Jamii.

Katika Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika Masuala uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana  pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa Makuzi kwa Vijana wetu.
Mbali na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
Pamoja na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa nia njema inakuomba wewe Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya nchi,Mashirika kusaidia Taasisi hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili vijana wetu wakue katika Makuzi mema na kujenga Tanzania ya kesho  iliyostaarabika.

 Blog Master

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...