Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo http://www.jakayafoundation. wapka.mobi/index.html.
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayo inamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulipa ada ya shilingi 37,000/=.
BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
BENKI KUU YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
Ugumu wa Maisha kipimo cha akili!
ReplyDeleteLakini akili zikizidi ktk kuyafikia malengo ya maisha unaweza kuchanganyikiwa ama ukafikia pabaya ndio kama haya hapa.
1.Kwa kweli Matapeli wana ujasiri!, kweli wamefikia kutumia taswira ya Raia Namba moja nchini Tanzania Jakaya ili kuhakikisha mkono unakwenda kinywani?
2.Baadhi ya aina za Ujasiri ni hatari sana, kwa kuwa unaweza kuzama kaburini moja kwa moja kama mtindo huu.
3.Maisha ni vile rahisi utakavyo yapeleka, haihitaji umiliki Masifuri mengi ndio utakuwa na uhakika wa maisha.
Tujipange na tuache kufikia malengo ya kimaisha kwa njia za mkato na zilizo hatarishi!!!
POLISI na IDARA YA USALAMA:
ReplyDeleteChukueni picha ya hao wanaoonekana ktk tovuti kwa chini
image:
http://akibasaccos.wapka.mobi/img/400365/400365820_becea42e67.jpg
Halafu watafutwe hao wenye sura hizo ili watoe ushirikiano (Sio kuwa wao ndio watuhumiwa lakini wanaweza kusaidia kuwapata wahusika kamili)
Wakuwawajibisha ni Mawakala waliosajili hizo namba za M-Pesa:
ReplyDelete0656-779278 (tiGO)
0766-422444 (Vodacom)
Hao Mawakala wanajulikana ktk Makampuni ya Mitandao, ni vile walitoa Taarifa zao walipoomba kazi za kutoa Huduma hiyo.
Hao watawajibika kuwataja ama kuwapata waliosajili hizo namba hapo juu ambao ndio Wahusika.
Hii njaa itatufikisha pabaya ingawa ni kweli ya kuwa Njaa haina adabu!
ReplyDeleteJuzi Jumatatu nilipigiwa Simu kwa Mobile Namba jamaa akidai yeye ni Afisa wa TRA.
La ajabu ananielekeza nionane naye sehemu ambayo hata Ofisi za Mamlaka hakuna!
Ktk Maongezi yetu kwenye simu aliponipigia aliniuliza maswali haya:
1.AFISA wa TRA:Wewe ndio Mkurugenzi wa Kampuni Fulani Fulani?
MIMI: Nikajibu ndio!
2.Afisa wa TRA:Unafanya biashara gani?
MIMI:Nikamtajia.
3.AFISA wa TRA:Inahitajika uonane na mimi una tatizo ktk Kodi zako.
MIMI:Nitakupata Ofisi gani kwa kuwa TRA wana Ofisi nyingi sana.
4.AFISA wa TRA:Ufike Mtaa wa Msimbazi na Swahili.
MIMI:Ofisi ninayojua ni MTAA WA KIPATA-TRA kwa kuwa hapo unaposema nina uhakika hapana Ofisi yeyote ya TRA!,,,mimi ninakuja moja kwa moja OFISI YA TRA MTAA WA KIPATA!
5.AFISA wa TRA:Akakata haraka simu!
Nilichokifanya moja kwa moja nikaenda Ofisi za TRA Kipata, la ajabu kufika pale nikaulizia Maafisa wote wakasema wala sikuitwa na PIA huyo mtu hawamtambui wala hamba yake ya simu hawaijui!!!
-----------------------------------
WANDUGU KWA MLOLONGO HUO WA MASWALI NA MAJIBU HAPO JUU PANA ELIMU INAYOHITAJIKA KUMTAMBUA TAPELI?
SWALI NO.1 Kwa nini atumie simu ya Mkononi?
SWALI NO.2 Kama yeye ni Afisa na anapiga simu kutoka Mamlaka wana ugeni gani kushindwa kuijua Biashar yangu wakati nilipoomba TIN na VAT nilitaja aina ya biashara?, huku ikiwepo ktk systems zao?
SWALI NO.5 Hapo alipotaja hakuna Ofisi za TRA na nilivyo mwambia nakuja huko Ofisini Kipata-TRA akakata simu!