Tamasha la sanaa za Ufundi la za Jukwaani lenye lengo la kupamba Siku ya Makumbusho Dunia limeanza rasmi katika viwanja vya Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Hadi sasa watu wengi wanazidi kumiminika ili kujifunza na kuburudika kwa njia mbali mbali za sanaa.

Matukio mbali mbali ya wanunuzi na wajasiriamali kama yanavyo onekana katika picha zilizo pigwa hivi punde.
Afisa Mkuu wa Raslimali watu wa Makumbusho ya Taifa Bw Fredrick Mwakalebela akimpongeza Bi Josephine Mpugusi wa TUFAFO ENTERPRISES kwa jitihada zake za ujasiriamali alizozianza mika 21 iliyo pita. Bi Mpugusi ameshiriki tamasha hili ili kuwakumbusha watanzania namana ya kupika Vyakula vya asili, kuvaa kiasili na kutumia mapambo ya kiasili.
Picha zote juu zinaonesha namna watu mbali mbali wakimiminika katika viwanja vya Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam mkabala na chuo cha IFM ili kujipatia bidhaa mbali mbali za asili. Picha habari na SIXMUND J. BEGASHE wa Makumbusho ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2013

    Mhhh picha ya mwisho huyu bwana muuzaji asipokua makini atatoa bure bidhaa anazouza,maana hilo tabasamu lake juu ya pozi la huyo mdada ni mashaka matupu.Kajisahau kwelikweli masikini da.Yaani muruwaaa, burudani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Hongereni Makumbusho ya Taifa, kwakweli ni jambo zuri sana mnalo fanya, Tanzania sasa inataka kupoteza Utamaduni wake. Tujitahidi kuurejesha. Mnatakiwa kuungwa mkono na serikali yetu na wadau mbali mbali waipandayo hii nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...