Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Josef Goeppel (Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani) mara Ujumbe huo ulipomtembelea Waziri kwa lengo la kujadili masuala ya uzalishaji umeme.
Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani wakimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes (wa kwanza kushoto) huku wakisubiri kuweka saini katika kitabu cha wageni Ofisini kwa Waziri Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia). Wanaofuatia kutoka kushoto ni Sabine Stuber, Marco Brulow, Josef Goeppel na Dorothea Steiner.
Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na Ujerumani katika kuzalisha umeme vijijini kwa kutumia nishati mbadala hususan upepo na jua.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani.
Ujumbe wa Wabunge hao uliongozwa na Josef Goeppel ambaye aliongozana na Dorothea Steiner, Marco Brulow, Sabine Stuber pamoja na balozi wa Ujerumani nchini Klaus-Peter Brandes.
Wabunge hao walimtembelea Waziri Profesa Muhongo ofisini kwake kwa lengo la kujadili naye namna Ujerumani inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha wananchi wengi kupata huduma za umeme hususan kwa waishio maeneo ya vijijini kwa kutumia vyanzo vya nishati mbadala.
Profesa Muhongo alieleza Ujumbe huo kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Ujerumani katika sekta ya nishati hususan nishati mbadala, katika jitihada zake za kuwapatia wananchi nishati hiyo.
“Sisi tupo tayari kushirikiana nanyi katika suala hili la uzalishaji umeme, kwani lengo letu ni kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika” alisisitiza Profesa Muhongo.
Naye Joseph Goeppel ambaye pia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge hao alisema amefurahishwa na namna Tanzania ilivyojipanga katika kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma ya umeme ambayo ni kichocheo cha maendeleo.
Aliahidi kupeleka ujumbe huo katika bunge la Ujerumani ili kuanza rasmi ushirikiano baina ya serikali hiyo na serikali ya Tanzania katika uzalishaji umeme kwa kutumia nishati mbadala.
Goeppel alimuomba Waziri Muhongo kuwa ushirikiano huo uanze mapema mwezi Januari baada ya kukamilisha taratibu zote za kiofisi zinazohusu ushirikiano wa kimataifa. Profesa alikubali ushauri huo na kusema Serikali ya Tanzania ipo tayari kuanza ushirikiano huo mapema iwezekanavyo.
ReplyDeleteEeh Mola tusaidie wenye nchi waliotukuka wakubaliane mapema juu ya hilo project ianze maana kwa maono yangu umeme wenye kigugumizi kinachozidi kila siku ni chachu kubwa inayopunguza kasi ya maendeleo ya nchini yetu na kuongeza umaskini kwa mwananchi wa kawaida
Mzigo Mkubwa abebeshwe Mnyamwezi!
ReplyDeleteNi suala muafaka sana jukumu hili akapewa Mjerumani sambamba na Mpango wa Mabasi yaendayo kasi DART Mradi kukabidhiwa Mjerumani pia kwa kujenga Miundo mbinu na Uendeshaji wake.
Ama kweli maendeleo tutayapata Miradi hii miwili ikiwa chini ya Big Brother mwenyewe Mjerumani.
Vishoka wa Tanesco kaeni mkipanga matambara yenu ktk Mifuko ya Rambo kujiandaa kurudi mkalime Vijijini!
ReplyDeleteNi vile siku zenu za Ulaji zinahesabika, je mtaweza kumchakachua Mjerumani?
Mafundi mjiandae na majembe mkalime!
ReplyDeleteItakuwa 'ni ajabu na kweli' kama mtaweza kumchakachua Mjerumani ktk suala la umeme.
Mafundi wa Karata 3 wa TANESCO mmeuona mwaka wa NJAA UNAVYOINGIA?
hehehehehe,
ReplyDeleteJeremani atakuwa anavaa ovaroli mwenyewe anafunga mita, kusoma mita na kupokea malipo.
Vishoka Tanesco ile Akaunti ya bahati iliyokuwa inamwagika manoti na kuwapa jeuri fedha na maisha kwenye mabaa na mitaani inafungwa muda si mrefu !!!
Muwanunulie wake zenu majiko ya mkaa na makarai ya kuanza kukaanga mihogo!
Itafaa Mjerumani aingie na Viboko mkononi akija Tanesco ili kukomesha wizi wa Mafundi na Makarani !
ReplyDeleteBwana amesikia kilio chetu!
ReplyDeleteMawakala wa kuunganisha Umeme wa Ofisi za mikononi, muandae Bustani za michicha na wake zenu muwanunulie makarai ya kuchomea maandazi!
ReplyDeleteUle Upatu wenu na Maafisa wa Tanesco umefikia ukingoni!
Ulaji umeota mbawa, heshima yenu itapukutika kama barafu muda si mrefu.
Ni kwa nini?
Mjerumani ameingia Tanesco!!!