Na Maelezo Zanzibar-18/05/2013 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameitaka Bodi na Menejiment ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuendelea na jitihada za kukiimarisha Chuo hicho ili kutoa Elimu bora yenye viwango vya kitaifa na kimataifa. 
 Rais Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalim Nyerere lililipo Bububu nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Amesema njia nzuri ya kupelekea kiwango cha ubora wa elimu chuoni hapo ni kuhakikisha Wanafunzi wanaojiunga wanakuwa na sifa zinazotakiwa pamoja na kupata Walimu wenye ujuzi. 
 Ameongeza kuwa ubora wa Elimu unaotolewa Chuoni hapo utawafanya Wahitimu kukabiliana na ushindani wa Soko la Ajira jambo ambalo litaweka heshima ya Chuo hicho. Aidha Dkt. Shein ameitaka Bodi ya Chuo kuandaa mikakati ya kuliwezesha Tawi la Chuo hicho kuwa Chuo kamili kinachojitegemea badala ya kubakia kuwa Tawi. 
 Amesema Utaratibu wa aina hiyo ndio unaofuatwa Duniani kote ambapo Matawi ya Vyuo vya Elimu ya Juu huwa yanaendelezwa na kuwa Vyuo kamili vinavyojitegemea. Dkt. Shein amewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kuitumia fursa waliyoipata ya kuwepo Chuoni hapo kwa kujikita zaidi katika masomo bila ya kujiingiza katika mambo yanayowapelekea katika malumbano. 
 Amewasihi Wanafunzi wa Chuo hicho kuendeleza maadili mema sambamba na kufuata Mila na silka zinazoendana na utamaduni wa kitanzania. 
 Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Dkt. John Magotti alielezea mafanikio ya Chuo hicho kuwa ni pamoja na kukamilika kwa Jengo hilo ambalo lina uwezo wa kuwahudumuia wanafunzi katika ngazi za Cheti, Stashahada na Shahada. Aidha alielezea changamoto zinazokikabili Chuo hicho kuwa ni pamoja na upungufu wa Mabweni ya kulalia Wanafunzi na Idadi ndogo ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hicho. 
 Amewataka Wanafunzi wenye sifa kujiunga na Chuo hicho na kuwataka Wazanzibari wenye ujunzi kuomba nafasi za ajira ikiwemo ufundishaji ili kukifanya Chuo hicho kuwa na sura ya kitaifa. 
 Awali akimkaribisha Dkt. Shein Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Dkt. Salim Ahmed Salim amewataka Vijana kuithamini Elimu wanayoipata Chuoni hapo ili iweze kuwa Mkombozi wa maisha yao.
 Jengo la Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililopo Bububu limegharimu Jumla ya Shilingi Bilioni 3.6 ambazo zimegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Tawi hilo ni kwa ajili ya Wanafunzi wa ngazi ya Cheti.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Dk. John Magoti, baada ya kuzindua rasmi  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Ardhi serikali ya Muungano Dk.Staulans Ntiyakunze,(wa tatu kulia) baada ya kuzindua rasmi  Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia meza na vikalio vyake wakati alipotembelea moja ya madarasa katika  Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo, baada ya kuzindua Chuo hicho,(kushoto) Mkuu wa Chuo Dk. John Magoti, na pili kulia makamo wa kwanza wa Rauis wa Maalim Seif Sharif,akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim.[
Mwalimu wa Darasa la Kompyuta Julius Maungo,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika darasa la kompyuta chuoni hapo
 Baadhi ya wanafunzi wa Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa chuo hicho leo 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea zawadi kutooka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere  Dk.Salim Ahmed Salim,wakati wa uzinduzi wa Tawi la Chuo hicho uliofanyika leo huko Bububu Nje ya Mji wa Zanzibar. Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...