Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linawashikilia watu wawili kwa Tuhuma za Unyanganyi kwa kutumia silaha na kujeruhi Mfanyabiasha wa Duka katika kijiji Cha Kitomanga Wilayani Lindi huku wakiwa katika hospital ya Mkoa baada ya kunusurika kufa kufuatia Wananchi wenye hasira kutaka kuwaua kwa kuwachoma Moto.

Akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake hii leo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga alieleza kuwa Watuhumiwa hao waliojitambulisha kwa Rajabu Juma Mbete(26) mkazi wa manispaa ya Lindi na Hamis Athuman(32) mkazi wa Mbembetini Kibiti Mkoani Pwani licha ya kupora simu 6 na fedha taslim laki 6 pia walimjeruhi kwa Mapanga Bw Hamis Hassan Muuza duka hilo.

Mwakajinga alibainisha kuwa Majambazi hayo yanayosadikiwa kuwa 4 walifanikiwa kukimbia baada ya Bunduki waliyokuwa nayo kugoma kufyetua risasi hali iliyofanya wanavijiji vya Kitomanga,Mkwajuni na Mbwemkuru kuanza msako na kufanikiwa kuwakamata na kuwajeruhi kwa kuwapiga na kuwachoma moto kabla hawajapata msaada wa Jeshi la Polisi.

Akielezea kuhusu kukutwa na risasi tatu za Shortgun,Bangi pamoja na Bunduki aina ya Shortgun ya kienyeji, Kamanda mwakajinga alifafanua Bunduki hiyo Ambayo hutumia risasi za Short gun pia walikutwa na risasi 3.

Kufuatia kukamatwa kwa majambazi hao baadhi ya Wafanyabiashara Manispaa ya Lindi akiwemo Seif Nasor na Ahmaid Nachuli wameeleza kuwa tatizo la kuongezeka kwa majambazi kunachangiwa na Uozo wa sheria hali inayosababisha jamii kujichulia sheria mkononi.

Watuhumiwa hao ambao wamelazwa huku wakiwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi watafikishwa mhakamani mara baada ya Afya yao Kuimarika kutokana kunusurika kuchomwa Moto na Wananchi ambapo tayari wameweza kutambuliwa na baadhi ya wanakijiji
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga akionyesha silaha iliyokutwa kwa majambazi hayo.
Hawa ndio watu wanaoshikiliwa na Polisi,baada ya kujeruhiwa na wananchi wenye hasira kali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2013

    Kwa Tanzania niijuavyo basi hata matibabu yao watu wenye kuhusishwa na tuhuma zozote zile huwa dhaifu mno na wengi hufa, kwa kifupi naweza kusema ni muendelezo wa kujichukulia sheria mkononi kama ambavyo wananchi hufanya.Ukiangalia picha tu hasa ya mmoja ya hao wahalifu aliyelala kitandani utapata jibu.

    ReplyDelete
  2. Che GuevaraMay 24, 2013

    Yes! safi sana raia! hadi raha! raia nawapa SHAVU kwa sana!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2013

    Rajabu na Hamisi,

    Hamkutumia nafasi nzuri ya kukaa na Wazee ilimpate msaada wa mawazo jinsi ya kukabiliana na maisha magumu.

    Badala yake mkakeba bunduki na kushiriki kazi mbaya sana ya fedheha na aibu ya Ujambazi.

    Mmeona sasa yaliyo wapata?,

    -Mlitaka kufanya Maajabu na Miujiza ya kumrusha BUNDI usiku wa Giza Kimazingaombwe (KUPATA FEDHA KUPITIA UJAMBAZI) ili mfikie malengo ya kimaisha, matokeo yake Bundi anawafia Mikononi!

    -Mlitaka kumchinja BUNDI usiku wa manane kama Sadaka (ILI KUTAMBIKIA KUUPATA UTAJIRI KWA NJIA YA UJAMBAZI), wakati Mwenyezi kamwe asingetoa ushirikiano ktk hilo...matokeo yake Kisu kikagoma kukata kooni mwa Bundi mkajikuta mnaangukiwa na Wananchi wenye ghadhabu na hasira kali!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...