Kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa mtu huyu ambaye ni omba omba akiwa amekaa katikati ya barabara ya Bagamoyo karibu kabisa na eneo la Victoria jijini Dar es Salaam, akiomba kwa watu wanaopita na magari katika barabara hiyo. Jambo hili si salama sana kwa mtu huyu kwani lolote linaweza tokea japo hatuombei itokee,hivyo ombi kwa wazee wa feva (wanausalama barabarani) kusaidia kumuondoa huyu mtu mahala hapa haraka iwezekanavyo.
Home
Unlabelled
Wazee wa Feva mmemuona huyu jamaa??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyu jamaa sio ombaomba ni kichaa. Alikuwa anasimama anatembea mbele kisha anageuza na kurudi, anaweza kufika tegeta kwa huo mzunguko. Sasa hv anakaa hapo barabarani. Alikuwa na manywele marefu sana na machafu naona wasamaria waliamua kumnyoa. Ni wakusaidia na kupelekwa hospitali.
ReplyDeleteHuyu jamaaa ndo kijiwe chake hapo victoria miaka nenda rudi hata wakimtoa kesho atarudi
ReplyDeleteWakati umefika kwa serikali kuanza kutoa "Benefit" kwa walemavu.
ReplyDeleteMdau wa BENEFIT umenichekesha na kunikumbusha mbali sana....kama huku uingereza kwenu mnakatiwa benefit itakuwa bongo?
ReplyDelete