Lori aina ya Fuso lenye nambari za usajili T 669 CEK likiwa limeigonga pikipiki iliyokuwa inakatiza kwenye taa nyekundu mapema leo katika eneo la Majumba sita njia panda ya Segerea.Waendesha pikipiki wengi wamekuwa wakiuendeleza uzembe huu ambao umekuwa ukifumbiwa macho sana na Watu wa Usalama Barabarani.
Huyu ndie dereva wa pikipiki hiyo akiugulia maumivu kabla ya kupatiwa msaada wa kukimbizwa hospitali.Picha na Adam Mzee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2013

    Waendesha Boda Boda hawafai kabisa. Hawafuati sheria yeyote. Kazi yao ni kupenya popote na kukaziza popote. Kila tundu au uwazi au upenyo ni halali yao pasipo hata kujiuliza kwa nini wenzangu wamesimama.

    Kibaya zaidi Siku hizo boda boda wanategemea madereva wa magari ndio wawalinde wao na kuwakwepa au kusimama ili kuwalinda boda boda. Taabu sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2013

    Wapo baadhi ya madereva wenye malori huwa na dharau sana kwa watumiaji wengine wa barabara, pia wapo vijana wa bodaboda ambao hawazingatii sheria za barabarani.Nafikiri pande zote mbili yapasa zielimishwe! Heshimu sheria, Heshimu wengine! Hayo hayatotokea.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2013

    hii Tz yetu inatisha sana . Watu wanamuangali badala ya kumsaidia hata huduma ya kwanza ?naona kila mtu amesimama tuuu , tutafika kweli ?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2013

    watamiuweni sana na huo ujinga mlioiga kwa wanageria eti pikipiki nayo imekuwa taxi

    acheni mambo ya kuiga watanzania pikipiki zinaua vibaya sana mtakuja kushangaa mwisho wa mwaka mkifanya hesabu zenu za vifo

    kipindupindu
    kifua kikuu
    malaria
    ukimwi
    ajali za mabasi
    ajali za bajaji
    ajali za bodaboda

    kwa mwaka tunaweza kujikuta watanzania zaidi ya milioni moja tumezikwa

    chonde chonde kwa wahusika wa ngazi hizo za usafirishaji simamisheni hizo leseni za bodaboda na bajaji.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2013

    Bodaboda ni janga la kitaifa. Vijana wengi wananunua bodaboda asubuhi jioni wamekwisha fuzu kuiendesha tena kwa kasi za wadudu na kubeba abiria.... Wao wanaimani waikiishaiwasha hiyo tukutuku yao huwa haina kusinmama na kwamba inaweza penya popote mara zote kama si nyingi wengi wa madereva hao ni feki wasiojua chochote juu ya sheria na kanunu za utumiaji wa barabara - Hayo ndiyo matokeo yake. Na yawezekana tunakokwenda yakatokea mengi makuubwa kuliko hili la leo. Tuwajibike sote else cha moto tutakiona.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2013

    Bado elimu ya usalama barabarani inahitajika sana kwa wote bila ya kujali aina ya usafiri,kwa kuwa hakuna asiyekosea.
    Lakini kitu cha muhimu pia ni UPENDO baina ya madereva maana kila mtu anajitafutia riziki.
    Maana sasa mtu haoni hatari kumburuza mwenzie kwa sababu zisizo na msingi.
    Tunakoelekea Watanzania siko tumesahau kuwa Taifa linajengwa na yeyote bila ya kujali kazi.TUWE WAZALENDO.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2013

    Tatizo kila jambo linawekwa kisiasa, hapa Tz ukipiga kelele kuhusu swala la taratibu na sheria mwingine atatokea na swala la ajira kwa vijana, bila kuangalia madhara gani yanaweza kutokea kwenye ajira hiyo. Ukitaka kujua uzuri wa bodaboda nenda mh2,utajua ama hospitali yoyote ya wilaya/mkoa uzilia takwimu za ajali za bodaboda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...