Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai ya rangi ya taifa) akiwa na Wajumbe wa Bodi ya Dinka Foundation ya Uholanzi. Asiye na tai ni Mhe. Leo Bellekom Mwenyekiti wa Bodi ya Dinka Foundation na mwenye tai nyekundu ni Mstahiki Drs J.Th. Jan Hoekema Mayor wa Wassenaar Uholanzi. Bodi ya Dinka na jiji la Wassenaar kwa pamoja Wanajenga shule ya msingi ya kimataifa ya Dinka Arusha. Hadi sasa wameishatumia Euro 224,000 na wanaendelea kutafuta fedha za kuendelea na ujenzi. Balozi Kamala amekutana na Bodi ya Dinka leo hii Uholanzi na kuishukuru kwa kazi nzuri inayofanya ya kutafuta fedha, kujenga shule ya Dinka na kutoa elimu bora kwa Watanzania. Mchoro ulioshikwa na Balozi Kamala unaonyesha shule itakavyokuwa ujenzi ukikamilika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Dinka Mhe. Leo Bellekom (mwenye kompyuta) akimueleza Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala mipango mbalimbali ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Kimataifa ya Dinka inayojengwa Arusha Tanzania. Kikao kimefanyika leo ofisini kwa Mstahiki Meya wa Wassenaar, Uholanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2013

    Swali la Kizushi/
    Ankali Michuzi kuna Uhusiano gani kati ya wewe na Ze-Tshirt yako na Huyu Balozi Kamala na Ze-Tai yake??
    Hii ya Balozi ni ile ile au ziko nyingi zinazofanana??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...