Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Klaus Peter Brandes amemshukuru Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ushirikiano aliompa kwa kipindi cha miaka miwili alichofanya kazi hapa nchini.

Ametoa shukrani hizo alipomtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake mapema leo Juni 7, jijini Dar es Salaam kwa nia ya kumuaga rasmi.

Akipokea shukrani hizo, Profesa Muhongo amesifu utendaji mzuri wa Wajerumani katika nyanja mbalimbali na kumwomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Serikali yake kuwa wanakaribishwa kuja kuwekeza nchini Tanzania katika miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme.

“Tunakaribisha kampuni za kijerumani zenye uwezo na zilizo makini kuja kuwekeza hapa nchini, hususan katika miradi ya umeme unaotokana na jua, upepo, majimoto na nishati mbadala,” amesema Waziri Muhongo.

Balozi Brandes anamaliza muda wake rasmi hapa nchini Juni 13 mwaka huu.
Balozi Klaus Peter Brandes (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), katika ukumbi wa mikutano wa wizara. Kulia ni baadhi ya maafisa wa wizara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    Mhesjhimiwa waziri,tafadhali angalia
    wema wako sio kila mwekezaji anafunguliwa mlango lazima uwe muwazi wa kuelezea taratibu za nchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...