Kutoka Kulia Bw. Nigel Shepherd, Mh. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Bi. Perez Ochieng, Balozi Peter Kallaghe. Waliosimama nyuma, Bw. Sam Ochieng (SACOMA), Bw. Hugh Morris na Bw David Smith.
Mh. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na msafara wake wakiondoka eneo la ghala la soko kuelekea mkutanoni. Kulia kwake ni Balozi Peter Kallaghe na Mkurugenzi wa SACOMA, Sam Ochieng.
Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akitoa shukrani zake na kuahidi uwezekano wa Tanzania kujitayarisha ipasavyo.
Ijumaa iliyopita itajulikana kama siku mlango mdogo ila muhimu sana ulipofungua kitasa chake kwa baadhi ya wananchi wanaojituma kikazi na kibiashara Tanzania. Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda alitembelea soko la mboga na matunda lililoko Leytonstone, mashariki ya London. Matembezi yalidhihirisha mahusiano ya ujirani mwema kati yetu Watanzania na Kenya yenye kampuni iliyoshajijenga ndani ya soko hili maarufu na kubwa sana.
Soko hilo linaloitwa Spitalfields si sehemu inayofahamika na wengi wanaoishi Uingereza licha ya kwamba jina hilo si rahisi kutamka au kuandikwa. Lakini Spitalfields (tamka “Spitol-fildz”), itakua eneo muhimu sana kwa vijana, wakulima na wafanyabiashara Tanzania, miaka ijayo.


,+Bw.+Hugh+Morris+na+Bw+David+Smith.jpg)



Thats why we need DUAL CITIZENSHIP guys. HII ITATUFANYA TUFANYE SHUGHULI ZETU KWA KUJIAMINI KABISA, ILA LA MSINGI NDUGU ZETU MLIOKUWA NYUMBANI YAANI WATANZANIA WOTE INABIDI MWENDE NA WAKATI ACHENI LONGOLONGO MAANA HIZO NDIO ZINAWACHELEWESHEA MAFANIKIO. TUWE NA TABIA YA KUFOCUS MBELE ZAIDI SIO MKITUMIWA VIJISENTI KIDOGO NA JAMAA ZENU WALIO NJE MKAAMBIWA MFANYE PROJECT HII AMA ILE MIOYO INAWAPASUKA MNAKULA HELA YAMENIKUTA NA YAMEWAKUTA WENGI TU. TABIA ILIYOPO MIONGONI MWENI MKIAGIZIWA FANYENI SHUGHULI HII NYIE MNAFANYA ILE THATS WHY MNAKOSA OPPOTUNITIES NYINGI KUTOKA KWA JAMAA ZENU WALIO NJE.JAMANI KILIMO KINALIPAAAAA TENA SANA! HAPA UK KUNA BAMIA, MIHOGO, NDIZI,MAGIMBI, HOHO,ZABIBU,EMBE, YAANI VYOTE TUZALISHAVYO NYUMBANI VIPO. KAMA GIMBI LINATOKA GHANA KWANINI TANZANIA ISHINDWE?! KAMA NYANYA CHUNGU INAKUJA TOKA INDIA WHY NOT TANZANIA?! HAPO MIE NDO NASHINDWA KUELEWA. KIFUPI HII EUROPE YOTE WATANZANIA TUKIAMUA KUILISHA TUNAWEZA ESPECIAL KWENYE MBOGAMBOGA NA MATUNDA!
ReplyDeleteNaungana mkono na wee annon hapo juu, mimi naishi east london, ukiangalia vyakula vinavyopatikana hapo vyote tunavyo Tanzania. tena niliona duka linauza miwa (sugarcane) kabisa, magimbi nilishangaa sana. Kwanini nasi tusiweze kafanya biashara.
ReplyDeleteHata ndizi hizi ndogo watu wanashangaa sana, lakini zinabei kubwa wakati nyumbani za kumwaga tu.
mimi nipo tayari kama kuna nafasi ya kuweza kupewa ruhusa na mikakati mizuri tuungane nasi tufanye biashara
asante
kweli kabisa naungana na wewe mdau wa kwanza.Ndugu zetu nyumbani wanatuangusha sana mimi yamenikuta hayo nimekuwa nikituma pesa nyumbani kwa nia ya kufanya biashara lakini ndugu wanakula pesa ukiuliza unapewa Kiswahili kirefu. Tanzania we hv everythin we can feed all Europe for sure. Yaan hata Uganda wanatupita wanaleta viazi vitamu, matoke hapa london while we hv all of this thing in TZ.Let be serious jamani tuache uvivu msituangushe ndugu zetu mlio nyumbani mkitumiwa vijisenti fanyeni mnachoambiwa kufanya.
ReplyDeleteTupeane mikakati ni vipi channel hii inaweza kufuatwa.Mi najiandaa kabisa kutembelea hilo soko.
ReplyDeleteviongozi wakitz bado hawajafunguka macho...wanafikiria ardhi...watakaa kama waethopia...tunahitaji dual citizenship...hatutaki kuambiwa porojo nyingi....ukitaka kupata na wao watoeeee.......
ReplyDelete