Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Basil Gadzios akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji cha Schweppes NOVIDA nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam Jumamosi Juni 8, 2013.
Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji cha Schweppes NOVIDA nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam Jumamosi Juni 8, 2013.
Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Basil Gadzios akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji cha Schweppes NOVIDA. Uzinduzi huo ulifanyika katika mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam Jumamosi Juni 8, 2013.
Kampuni ya vinjwaji baridi ya Coca-Cola leo imezindua kinywaji kipya cha Schweppes NOVIDA ambacho kinapatikana kwenye chupa ya kijana ikiwa na KAULI MBIU, ‘Ishi Maisha Mazuri’. Kampuni ya Coca-Cola imedhamiria kuifanya bidhaa ya Schweppes NOVIDA kuwa kinywaji cha kisasa kwa watanzania wote wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.
Schweppes NOVIDA imetengenezwa kukidhi ladha na mahitaji ya wateja wa rika zote. Kinywaji hiki kinapatikana katika ladha mbili – CHENZA (Mandarin Cooler) na NANASI (Pineapple Breeze).
Schweppes Novida inapatika nchi nzima kwenye chupa ya kawaida yenye ujazo wa 300ml na ya plastiki yenye ujazo wa 500ml kwa bei ya reja reja ya Tshs 600 na Tshs 1000.
Kinywaji cha Schweppes NOVIDA kitafanyiwa matangazo na kutambulishwa kwa wanywaji kupitia magazeti, mabango ya barabarani, radio na TV. Matangazo hayo yatakuwa yakionyesha jinsi ya Kuishi Maisha Mazuri kama maudhui ya kinwyaji chenyewe. Matukio, sehemu za mauzo na muonekano wa digitali utasaidia kuhamashisha wateja kupenda Scheppes NOVIDA na ladha yake katika muonekano kwenye chupa mpya.
Kauli mbiu ya Schweppes NOVIDA, Ishi Maisha Mazuri ni ya kisasa, mpya na yenye nguvu mpya. ‘Karne za zamani, Amerika ilikuwa ndio ‘dunia mpya’ iliyojaa yanayowezekana tu. Kwa dunia ya sasa, kila kitu kinawezekana.
Hivi leo uwezekano wa maisha mapya, mwanzo mpya, na utaalum ziko kila sehemu tunayoiona. Na ndoto ya Afrika imekuwa ya kweli. Ukizingatia hayo, kampuni ya Coca-Cola leo inazindua kinywaji ambacho kitakupa kile unachohitaji na kukufanya uishi maisha ya kisasa na kuwa na ndoto ya kila siku ya Kiafrika’. Anasema Maurice Njowoka, Meneja Bidhaa Coca-Cola Kwanza Tanzania.
Kinywaji cha Schweppes NOVIDA ni mahsusi kwa kila mtu, cha kisasa na kila mtu angependa kuonja ladha yake. Ni kinywaji cha watu makini na wenye kutawala maisha yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...