RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AMEMTEUA FARAJI SHOMARI JUMA KUWA MWENYEKITI WA MAHAKAMA YA ARDHI ZANZIBAR.
UTEUZI HUO AMEUFANYA KWA MUJIBU WA UWEZO ALIOPEWA CHINI YA KIFUNGU NAMBA 4(1) CHA SHERIA YA MAHAKAMA YA ARDHI NAMBA 7 YA MWAKA 1994 KAMA KILIVYOREKEBISHWA NA SHERIA NAMBA 7 YA MWAKA 2008.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI AMBAYE PIA NI KATIBU MKUU KIONGOZI DKT. ABDULHAMID YAHYA MZEE UTEUZI HUO UNAANZA JULAI 10 MWAKA 2013.
AIDHA DKT. SHEIN AMEFANYA UTEUZI WA MAKADHI WATATU WA WILAYA KUPITIA UWEZO WA KISHERIA CHINI YA KIFUNGU NAMBA 5 CHA SHERIA YA MAHKAMA YA KADHI NAMBA 3 YA MWAKA 1985 KAMA ILIVYOREKEBISHWA NA SHERIA NAMBA 4 YA MWAKA 2003.
MAKADHI HAO NI PAMOJA NA SHEIKH OTHMAN AME CHUM, SHEKH ABDULRAHMAN OMAR BAKAR NA SHEIKH KHAMIS KASSIM HAJI.
UTEUZI WA MAKADHI HAO UMEANZA JUNI 06 MWAKA HUU.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Ingepedeza zaidi kama ingewekwa picha ya huyo aliyeteuliwa kuliko hii ya Rais Shein!!
ReplyDelete