Dear Ankal
Kwa kweli wajumbe wa tume ya katiba wameyatendea  haki maoni ya watanzania  juu ya katiba  mpya. Ingawa  sijapata  muda  wa kusoma  kifungu hata kifungu kwa  utulivu, lakini kwa muonekano wa  awali  rasimu ni  nzuri  na itahitaji marekebisho machache  ya kimsingi.  Rasimu ya  katiba  imependekeza kuwepo kwa  serikali tatu, yaani ya  Muungano, ya Tanzania zanzibar(ambayo ipo kwa sasa) na ya Tanzania Bara( ambayo katika  katiba ya zamani imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania). Kwa  utaratibu wa tume rasimu ya katiba itajadiliwa katika mabaraza mbalimbali yalioundwa katika ngazi tofauti na baadae kwenye  bunge la katiba  na mwishowe itapigiwa kura ya maoni na itakuwa tayari mwaka 2014. Serikali , inataka   katiba hii ianze  kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2015.
 
Angalizo langu:
Iwapo  katiba hii  itapita katika mchakato mzima na ikakubalika kwa wananchi kwamba  tuwe na serikali tatu. Serikali  ya Muungano itakuwa na katiba, Serikali ya Tanzania Zanzibar  wanayo katiba yao, Serikaliya  Tanzania bara itakuwa haina katiba yake, hivyo basi  tutabidi  tuanze  mchakato mpya  wa kupata  katiba ya serikali ya Tanzania bara mwaka 2014. Hili linaweza  kuchukua muda mrefu na pengine kuchelewesha au  kuhairisha  uchaguzi wa mwaka  2015.
 
Sijui serikali na wanasiasa wanaliangaliaje  hili.
Wadau wa Globu ya Jamii je mna mawazo gani  kuhusu angalizo hili?


Mdau wa KATIBA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Serikali tatu ni mzigo kwa Wananchi wa Tanzania Sio Jambo la kushabikia hata kidogo, Katiba bora ni ile itakayoleta unafuu kwa Wananchi wa Taifa husika, kwa kipindi cha Muda mrefu huduma za Afya, Elimu na Miundombinu mingi imekuwa ikitengewa fedha kidogo kutokana na ufinyu wa Bajeti, sasa mfumu wa Serikali Tatu, maana yake hata ile bajeti ndogo itatumika kwa Ajili ya kuendesha Serikali badala ya kuleta Maendeleo. Ni vyema tuwe na Serikali Moja ambayo itakidhi mahitaji ya wananchi, ambayo itaboresha huduma muhimu pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi kwa Wananchi.

    Rasimu ya Katiba, itawanufaisha wanasiasa wanaotaka uongozi, na Si wa Wananchi weye kiu ya Maendeleo.

    TUSEME HAPANA KWA SERIKALI TATU, TUNATAKA SERIKALI MOJA, NA HIYO NDIO MAANTIKI YA KUUNGANA KWA NCHI MBILI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    mie nakubaliana na mdau wa hapo juu kabisa,kwamba itakuwaje nchi mbili ziungane halafu kupatikane marais wa tatu? kwanini kusiwe na serikali moja ? tu tumeungana kivipi sasa mbona sielewi? kila mwaka nchi ndogo itakuwa inafanya kutafuta viongozi wa ngazi mbali mbali kutokana na kuwepo kwa madara sana,mie naona hapo serikali moja tu basi ,kama haiwezekani wapeni zenji nchi yao bana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    na sisi wazanzibari tunasema hatutaki serikali mmoja tunataka mbili kwa sababu tulivyo ungana tulikuwa serikali huru na kwanini tupoteze uhuru wetu kwa ajili ya kuungana

    watanganyika tafuteni serikali yenu

    msidhani sisi wajinga tumekaa kimya lakin tuna jua kutafakari kwa kina kirefu sana


    tumechoka kutawaliwa tuna taka taifa letu huru lenye heshma na hadhi ya nchi huru hatutaki muungano tena

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2013

    kila mtu anamtazamo wake. Serikali tatu ni kuwadanganya wazanzibari kwa kifupi. Hio serikali ya muungano na ya tanganyika imechanganywa humo humo ktk serikali ya sasa ya muungano.
    Na ikiwa hizo wizara muhimu ambazo wazanzibari hawataki ziwe kwenye muungano bado zitabakia kwenye serikali mpya muungano , basi hakuna haja ya kuwa na serikali tatu.
    Tunasema tena hatutaki muungano kila mtu awe na serikali yake , tuwe na ushirikiano tu kama vile tunavyoshirikiana na uganda , kenya nk. Hawa kina warioba wasidanganye wazanzibari bure wanajidanganya wenyewe , wenye macho hawaambiwe watazame. Wenye akili ni wengi lakini maarifa ndio tatizo , tunakuomba warioba na tume yako chukueni wenyewe hio katiba. Na kama waadilifu basi tuipigie kura. waznz hawataki muungano basi mmetushika tuuuu , heee

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2013

    Kusema kweli kwa rasimu hii bado ni danganya toto ila WAZANZIBAR waleo sio wa jana hakuna mzanzibar mjinga akubalie kuburuzwa tena tushachoka kila siku kupangiwa tunataka tujiendeshe wenyewe hio rasimu ni usanii tu wa kutaka kuendelea na katiba hii hii kwa sababu wanajuwa hakuna atakaekubali huo ujinga wao na mara hii ni mwisho ikishindikana kukubaliana na kile tukitakacho mamlaka kamili zanzibar mamuzi magumu tutakayoyachukua potelea mbali :LIKITOTA NALITOTE : KWANI LAZIMA TUUNGANE TUSHASEMA HATUTAKII HEBU TUACHIENI NA KIJINCHI CHETU .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...