Ankal Misupu mzee wa saundi. 

Wasalaam aleuikum

Ankal, mimi ni mdau blogu yetu ya jamii wa long taimu xana. Yaani wa siku nyingi kinoma. tangu globu ya jamii inazaliwa bado kichanga vile, nilikua naipakata. Na ki computer changu cha henzi hizo na dial-up, ilikuwa ni lazima niichungulie blog ya jamii mara tatu kwa siku, nitupe komenti mbili tatu za uongo na kweli nianze kucheka vituko vya Peter Nalitolela wa muzumbe univesiti. unaona
 
Ankal mimi ndo watu wa mwanzoni wa kukomenti kwenye globu yetu. ila leo, nalazazimika kuchukua fursa hii kutoa dukuduku moja tu. Globu ya jamii imebadilika Kuna vitu ambavyo vimepotea na tunavimisi sana. Tumemisi ze- fulunazz ya Ankal, tumemisi konoz za ankal, tumemisi nondozz za mzee wa Oxford, mbishi ngangari us-Blogger, Debates na nondoz zilizoenda shule za economy of walsstreet, Prof.John  Mashaka na Dr. hidleband Shayo.  tumemiss Salamu za Mtu mzima Baraka wa Chibiriti wa inter milan, huko Cessnia , Mzee wa vitu vitamu vya uhakika, za italy, ma Spania, mzee wa menyu, Chef Issa,  na taswira za ankal akiwa vekesheni huko maju. unaona, yaani listi ndefu

  itakuwa vizuri sana, you know, kama vipi,  ukiwaita hawa waasisi waendeleze libeneke. Au ndio wamekuwa Zilipendwa ma classic? Ankal hawa jamaa walichangamsha sana genge. Globu ya jamii ilikuwa ni kijiwa cha kujiburudisha na kujielemisha. Tunaokaa ugenini bila marafiki, globu yetu ndiye rafiki mkubwa tuliyekuwa naye.  Hasa peter nalitolea, Ze fulanazz, US blogger na John Mashaka, Ze Konozz. Tunaomba warudi walikuwa ni entertainers na stress relieves wakubwa sana

Mdau. J Chingwile-
mamtoni , olimpia ugiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2013

    Ha ha ha ha ha ha ha ha ha
    Mzee umeniacha hoi. Kweli michuzi enzi hizo genge lilikuwa linachanga msha sana. wakina Mashaka ndio pioneers wa blog ya jamii.walikuwa wanachangamsha sana. inabidi warudi watuburudishe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2013

    wewe mzee wa olimpia napenda tu kuuliza, huko ugiriki unafanya kazi gani ambayo hata shule umeshidnwa kwenda umebakia kuandika kiswahili kischoeleweka? rudi shule kama haukufukuzwa na wagiriki wenye hasira

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2013

    Nakubaliana na mawazo mengine ya ndugu yangu hapo juu.Lakini pia natambua kuwa.. the beat goes on...twapenda kuona yale tuliyoyazoea lakini twapenda maendeleo.Nafikiri shida ya Misupu ni utambuzi wa nini ni nini.Hata hivyo mimi bi nafsi namiss fulanaz hasa itokapo nje ye nchi, kwenye likizo, nafikiri imeuzwa,au inatia aibu kwa kuwa na viraka. Kisha jamaa vipi watuletea ngoma uzipendazo,twaomba tudokozee zile zinazokukera.Sijitapi lakini blog imekuwa kama main connection yangu na bongo, na hapana siku yapita bila kuchungulia mara sita au saba hivi.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2013

    Yaani kukaa kwako ughaibuni wiki mbili ndio unajifanya hata Kiswahili kinakupiga chenga!!!!

    ReplyDelete
  5. MDAU KILIO CHAKO KIMESIKIKA, KAA MKAO WA KULA. NA ASANTE KWA SAPOTI YAKO WEWE NA WADAU WENGINE NGULI...

    ReplyDelete
  6. DR. TULANGIYEJune 03, 2013

    IDEA MICHUZI, TUNAKUBALIANA NA MDAU. WARUDISHE WAKINA JOHN MASHAKA NA US BLOGGER. YAANI PALE ILIKUWA NO KAMA MECHI KATI YA MAN-U NA CHELSEA. TUNAOMBA WARUDISHE HAO WAKUU WAWILI. YAANI WAO NO NOMA. TRAFIK WALIYOLETA ILIKUWA KUBWA SANA

    ANKAL, KAMA ZE FULANAZZ , MIMI NIKO TAYARI KUDHAMINI TURUDIE ENZI ZETU.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2013

    wadau, John Mashaka siyo binadamu, huyo no jina bandia la kimkakati ankal alijitengenezea kuwavutia wasomaji. Haiwezekani binadamu mmoja kuwa na akili kiasi kile.

    Huyu Mashaka wa michuzi Ni watu mbali mbali, wataalamu mbali mbali wa lugha ya kiingereza na uchumi kuandika miss tofauti na kupost. Huyo Mashaka wanayemsema site. Yeye anafanya kazi ya investment banking walstreet Hana uwezo kuandika makala kama Yale.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2013

    Wewe Mdau wa Ugiriki:

    Sina sababu ya kuuliza unafanya kazi gani huko kuliko yumba Uchumi na Misha kwa ujumla, isipokuwa ni bora urudi Mtwara pana matarajio ya gesi kunufaisha wananchi badala ya kubakia huko Ugiriki.

    Ni vema ukadai mahitaji yako ukiwa tayari upo Newala-Mtwara Tanzania!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    Mdau wa umangani ugiriki tumewamisi pia watoto mbwa aka ffu au ngoma afrika band na madongo yao

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2013

    Kweli kamanda Ras Makunja na FFU kiasi wameuchuna,mara ya mwisho tulisikia kuwa nyumbani kwa kamanda
    kumeibiwa bundi !
    ndio kusema hapakuwa na ulinzi wa kutosha katika himaya ya mkuu wa kikosi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...