
Jifunze Kuimba na Joett CD Yazinduliwa
Joett, mwalimu wa kuimba na jaji katika kipindi
cha TIKISA kinachorushwa ITV, ameachia CD ya
kujifunzia kuimba ijulikanayo kama Jifunze
Kuimba na Joett.
Mazoezi hayo ya kuimba
ambayo yalianza kurekodiwa mwaka 2010 na
kumaliziwa Machi 2013, yanamchipuko wa singo
yake I Could Never Live (Without Your Love),
ambayo iliachiwa mwaka 2010/2011.
Joett aliandaa
mafunzo hayo pamoja na mpiga kinanda mahiri Luigi
Tamburi, ambae miaka ya nyuma alikua mpiga
kindanda wa concert jijini New York, Marekani. Joett,
ambae singo yake mpya Color Me Beautiful
inamahadhi ya miondoko ya disco la miaka ya 70,
alisema,
“Nilitaka kuandaa mafunzo ambayo ni
kamilifu na yanayotumia irabu pamoja na mashairi
kwenye mpangilio wa kujifunza kuimba. Kwa kawaida
mafunzo ya kuimba hutumia irabu. Lakini mimi
nilitaka kutengeneza mpangilio ambao una mashahiri
pia, ili iwe rahisi na haraka zaidi kutumia ujuzi huo
kwenye wimbo wowote”. Maelekezo kwenye CD hiyo
ni kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
“Naamini huu utakua mchango wangu mkubwa
wakukuza vipaji hapa nchini ili vijana wetu waweze
kujiendeleza katika fani hii,” alisema Joett. “Kwa
kutumia mazoezi haya katika miezi michache iliyopita,
nimeweza kurekebisha sauti za wanafunzi wangu
kwa urahisi zaidi,” Joett aliongeza.
Kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, Joett huandika
ushauri kuhusu maswala ya kuimba kwenye blog lake
joettmusic.com, na baada ya kuachia hiyo CD ya
kufundishia kuimba tarehe 16 Mei 2013, Joett yuko
tayari kusaidia jamii kwa kujibu maswali na kutoa
ushauri kuhusu maswala ya uimbaji, kupitia vipindi
vya redio na televisheni vya hapa nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...