Kikao cha kawaida cha kamati ya pamoja kati ya Viongozi na wataalamu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kimekutana kujadili changamoto mbali mbali zinazoleta kero katika masuala ya Muungano.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal alikiongoza kikao hicho akiambatana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma.
Akiwasilisha masuala yaliyofanyiwa kazi kufuatia agizo la kikao kilichopita Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri anayeshughulikia masuala ya Mauungano Mh. Samia Suluhu Hassan alisema ipo hatua kiasi iliyofikiwa katika kushughulikia masuala hayo zikiwemo zile kero zinazoleta changamoto ndani ya Muungano.
Waziri Samia aliyataja masuala hayo kuwa ni pamoja na Ushirikia wa MIRADI YA Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, suala la mafuta na Gesi kutolewa katika mamabo ya Muungano, Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za nje katika mfumo wa uhusiano wa Kimataifa, Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Ajira za utumishi wa wafanyakazi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano.
Alisema majadiliano ya wataalamu na viongozi teule wa pande zote mbili katika masuala ya Mafuta na Gesi pamoja na lile la Uvuvi wa Bahari kuu yemechelewa kutokana na ufinyu wa bajeti za vikao hivyo.
Hata hivyo alifahamisha kwamba hatua za majadiliano hayo zitaendelea ndani ya kipindi cha miezi miwili inayofuata kwa vile mfuko wa kuratibu vikao hivyo tayari umeshapatikana.
Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Abdulla Juma Abdulla akizungumzia suala la ushiriki wa Miradi ya Zanzibar ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki inasubiri uchambuzi yakinifu katika miradi ya Bandari ya mpiga Duri Unguja, Uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na Chelezo cha Malindi Unguja.
Mh. Abdulla alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika { ADB } kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki imekusudia kusaidia mradi wa Bandari ambao tayari makampuni matatu ya kimataifa yalijitokeza kufanya uchambuzi huo.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Viongozi na watendaji wa pande zote kwa juhudi wanazoendelea kuchukuwa za kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo.
Balozi Seif alisema akiwa kama mtendaji mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amekuwa na mawasiliano ya kirafiki zaidi kati yake na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda wakati inapotokea hitilafu ya utendaji baina ya pande hizo mbili.
“ Tumekuwa tukiwasiliana na kushirikiana kwa karibu zaidi kama ndugu mimi na Waziri Mkuu Mh. Pinda wakati yanapojitokeza matatizo ya utekelezaji wa majukumu katika pande zetu mbili. Na hili wakati mwengine tunalazimika kuwasiliana kwa simu wakati wowote hata kama usiku “. Alisisitiza Balozi Seif.
Akikiahirisha kimao hicho cha Kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabr Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Mohamed Gharib Bilal amewaasa Watendaji wa pande zote mbili kuhakikisha kwamba wanakuwa makini wakati wote katika kukabiliana na changamoto zinazojichomoza katika masuala ya Muungano.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/6/2013.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moha Gharib Bilal akiendesha Kikao hicho kilichokutana katika Ukumbi wa New Dodoma Hoteli Mjini Dodoma.Kushoto ya Dr. Bilal ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na upande wake wa kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ waliokutana katika ukumbi wa New Dodoma Hoteli Mjini Dodoma katikakikao cha kawaida cha kuzungumzia masuala ya Muungano na change moto zinazokabili Muungano.
Waziri wa Nchi Omfisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee akifafanua masuala yua fedha katika mkutano wa Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ Mjini Dodoma.




huu ni usanii tu na matumizi mabaya ya kodi za wananchi ati tanganyika ndio imejifanya Tanzania na kuiacha zanziba kama mtoto yatima si kila nchi ifanye mambo yake bila ya interfere no more interferer.hatuutaki muungano wenu huo wa kuidhulumu zanzibar ivo hamfahamu kama hamfahamu tutakufahamisheni kwa maneno na kwa vitendo dhulma tu.sisi wazanzibar bila ya mamlaka kamili ya nchi yetu patachimbika hilo mlijuwe
ReplyDeletewazanzibar hatutaki muungano na nchi yeyote mbona wakaidi nyinyi ccm tunataka mamlaka kamili ya nchi yetu hii vifuu undu hivi
ReplyDeletehatutakiiiiiiiiiiiiiiiiii tuachiwe si kila nchi iwe na mamlaka yake mnatulazimisha hatutakiiiiiiiiiiiiiiiiii
ReplyDeletehii kamati ya ajabu , ina harufu ya rushwa pengine sitting allowance tu hapo iko kwenye mammilioni kwa kichwa , unafikiri hao wajumbe wataangalia manufaa ya waznz au matumbo yao? watu muhimu haawamo kwenye hii kamati kama sefu sharifu na ismail jussa ambao hawawezeki kupewa rushwa mbele ya maslahi ya znz
ReplyDeletePinda ndio source ya matatizo yote lakini hilo halionekani,zanzibar sio nchi,imezua mtafaruku kwa muungano mzima,serikali imechoka,hili tatizo lengine kama imechoka iko haja gani kuwapiga wananchi ikiwa mmeshindwa kiwaunganisha wananchi kisiasa ni bora kuachia ngazi,na kuwaachia ambao hawakuchoka kulishughulikia suali la mtwara -lakini mimi nasema kwa mtwara mengi yatakuja ni bado mapema na mazito ,na kila mmoja atatia akili kama hamnazo.
ReplyDeleteKero za muungano hazitaisha mpaka muungano wenyewe uishe .
Ikiwa rasimu ya muungano iko wazi kila mmoja wetu kuiona na kuijadili basi na katiba ya muungano ya 1964 iwepo wazi pia ili tuifananishe nayo na kuweka mambo sawa ,sasa mnaficha nini,kanzu mpya uko uwanjani na ilikwisha iwepo uwanjani tuione tunajenga wapi na kubomoa wapi lakini hapana hamfanyi hivyo jiba la roho limekukaeni kama hamtalitoa jiba hili litawatoa roho.
hao viongozi wetu hapo juu huyo wa kulia na kushoto ni mahendsamu sana mwe! ukiwaachia mtoto mchanga atalia mpaka urudi kisimani.
ReplyDelete