Kutoka kushoto, katibu mkuu ofisi ya makau wa raisi bwana Sazi Salula, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano mh. Samia Suluhu Hassan, mwenyekiti wa mkutano,Mh Ali Juma shamhuna waziri wa Elimu Zanzibar, akimuwakilisha Wazri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais zanzibar kama mwenyekiti mwenza katika kikao cha kamati ya pamoja cha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi zanzibar cha kujadili changamoto za Muungano.
Baadhi ya mawaziri wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano mjini Dodoma Leo
Baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya makamu wa rais wakifuatilia mazungumzo katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano kinachoendelea mjini Dodoma. Picha zote na Evelyn Mkokoi
hivi jamani nyie mlokaa kwenye hicho kikao chenu mnamuwakilisha nani mbona mnajitoa fahamu hichokikao ni cha ccm ,hivi ccm ndio wenye hati miliki ya tanganyika na zanzibar .nendeni Dodoma ,butiama mpaka mnakokujua nyinyi sisi wazanzibari haturudi nyuma katu kuntu tumechoka na ufisadi wenu a kuifisidi zanzibar ,msimamo wetu ni ulule bila ya mamlaka kamili ya kila nchi tutaendelea kuidi kwa nguvu zetu zote nchi yetu ya zanzibar mpaka tone la mwisho la damuzanzibar si ya ccm wala si ya sheni ,sefu ,shamhuna ,salim na iddi, nahonda,jussa au samiya, zanzibar ni ya wazanzibari wote pemba na unguja.tuheshimiane kila kiumbe kina haki yake na kila nchi ina watu wake na haki zao. mamlaka kamili zanzibar na mamlaka kamili tanganyika hakuna kuhangaishana hapa tumechoka na ubabaishaji wenu. kwa mfano zanzibar kuna serikali ya umoja wa kitaifa mbona hamjawashirikisha viongozi wa upande mwngine huo ndio ulaghai wenu tusoutaka mpaka kieleweke hatusiki cha muadhini wala mteka maji msikitini zanzibar huru na tanganyik huru uwo upumbavu wenu mbona haupo kwenye nchi zote za afrika iwre kwa zanzibar tu muélala doro .kama mtatupiga kama mlivyosema huko bungeni au mtatuuwa tushazoea msimamo pale pale .zanzibar daima na itadumu madikteta wakubwa lakini tutapambana kwa hoja wazanzibar wa miaka ya 60 sio wa sasa acheni udikteta huo
ReplyDeleteAcha kutoka povu wewe. Hakuna mtanganyika anayeutaka muungano wenu.
ReplyDelete