Kilele cha tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Music Awards kinatarajia kufanyika siku ya Jumamosi, Juni 8 katika ukumbi wa Mlimani City kwa kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2012. Kwa mara ya kwanza mwaka huu kutakuwa na tukio la Red Carpet ambapo watu maarufu watapita kupiga picha na kufanya mahojiano ya moja kwa moja na muendeshaji ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo.

Tuzo hizi zitaonyeshwa live kupitia katika mtandao wa Internet huku watumiaji wa simu za mikononi na kompyuta wasioweza kufuatilia kupitia TV zao wakiweza kutazama mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager (www.facebook.com/kilimanjaropremiumlager) na pia mtandao wa LIVESTREAM (http://new.livestream.com/KTMA2013/live) .

Wakati wa zoezi la utoaji tuzo washindi wote watapata nafasi ya kuongea na kuwashukuru mashabiki katika Social Media Lounge itakayoendeshwa na Millard Ayo kutoka Clouds FM na Sam Misago kutoka East Africa TV. Picha za matukio na kinachoendelea katika ukumbi wa Mlimani City zitakuwa zikirushwa moja kwa moja katika mtandao wa Twitter na Instagram ambayo ni ( @Kili_Lager).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...