Ndugu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wakazi wa kijiji
cha Malangali,Kata ya Luduga,Wilaya ya Wanging'ombe mapema jana jioni.Kinana alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo na suala la mgogoro ardhi
uliohusu wananchi waishio eneo la hifadhi ya Malangali kuhamishwa,Kinana
aliishauri serikali kulifanyia kazi jambo hilo kwa umakini mkubwa,
kuondoa mgongano na usumbufu kwa wananchi,Aidha katika mkutano huo
hadhara Kinana aliahidi kiasi cha fedha kwa vijana
kuwawezesha kuunda umoja wao wa kufanya shughuli mbalimbali za
kimaendeleo.
Maelfu ya wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (chini ya bendera) alipowasili jana, kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Wanging'ombe, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya udongo kwenye ujenzi wa zahanati ya Samaria, Kata ya Makoga Wilaya ya Wanging'ombe alipopita eneo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Chdm mkisaidiana na Mhe. P. Msigwa mkachane mbao msituni!
ReplyDeleteIringa yote na Wanging'ombe hizoooo mikononi mwa CCM