TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kila Jumatatu kuanzia saa 4 Asubuhi limekuwa likiendesha ‘Jukwaa la Sanaa’ kwenye ukumbi wake ulioko makao makuu ya Baraza Ilala Sharif Shamba.

Katika jukwaa hilo linalohusisha wadau wote wa sanaa, hoja nzito na motomoto kuhusu tasnia ya Sanaa na Utamaduni zimekuwa zikijadiliwa na kujibiwa.

Katika kuelekea urasimishaji wa Sekta ya Filamu na Muziki ambao ulianza rasmi tarehe 1/01/2013, ifikapo tarehe 01/07/2013 hakuna kazi yoyote ya Filamu na Muziki itakayoingia sokoni bila kuwa na stamp ya TRA. 

Baraza la Sanaa katika Jukwaa la Tarehe 03/06/2013 litazikutanisha taasisi zote nne zinazohusika na urasmishaji ili kutoa elimu kwa Wasanii, wadau na wakuzaji sanaa kuanzia saa 4 :30 Asubuhi. Wadau wa sekta ya sanaa mnakaribishwa kuleta michango na hoja zenu ili kuleta mustakabali utakaojenga sekta ya sanaa. Taasisi zinazohusika na Urasimishaji wa sekta ya sanaa ni:

  1. Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
  2. Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA)
  3. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
  4. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

WOTE MNAKARIBISHWA

Godfrey Lebejo Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI, BASATA

Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to The Executive Secretary
BASATA Arts Centre, 
Ilala Sharif Shamba, 
P.O. Box. 4779, 
Dar es Salaam, 
Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485, 
Fax: 0255 - (022) - 286 0486 
E-mail: info@basata.or.tz Website: basata.or.tz



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2013

    Hii ina mana wasanii wataanza kulipia kodi TRA? Mbona watakoma! haya pia kuhakikisha hawatapeliwi ila zitatokea stamp fake za TRA na filamu zitauzwa, kibongobongo.Kila la heri waandaaji wa filamu Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...