Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akifungua
mafunzo ya siku moja kwa Madiwani kuhuisiana na Sheria ya Maadili ya
Viongozi Wa Umma.
Kamishna wa Maadili Jaji mstaafu Salome Kaganda
akitoa taarifa fupi ya Sekritereti ya Maadili ya Umma kwa Madiwani wa
Halmashauri ya wilaya Kilwa.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakiwa katika mafunzo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Ya Kilwa Abdallah
Ulega akiwa katika picha ya Pamoja na Kamisshna wa Maadili Jaji
Mstaafu Salome Kaganda na Madiwani wa Halmashauri ya Wiaya ya Kilwa
waliohudhuria mafunzo ya Maadili katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo.
Picha na Habari na Abdulaziz Video -Kilwa.
Madiwani Nchini wametakiwa kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kusimamia
maadili katika maeneo yao pamoja na Halmashauri kwa kuwa karibu na
Wananchi ikiwa pamoja na kutatua kero zinazowakabili badala ya wao
kujiona ni sehemu ya Halmashauri pekee.
Akifungua semina ya Mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya
Kilwa kuhusu Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma,Mkuu wa Wilaya ya
Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega alieleza kuwa ili kudumisha
demokrasia na Utawala Bora na kuimarisha imani kwa Jamii ni Vema.
Viongozi kusimamia Utekelezaji wa sheria maadili ikiwa Pamoja na
Ujazaji wa Tamko linabainisha na Rasilimali Ulizonazo
Aidha Ulega aliwataka Madiwani hao kutoa Maamuzi sahihi kwa kufuata
sheria ,Kanuni na taratibu kwa kufuata Miongozo na ikiwa Pamoja na
Kubainisha Mali alizonazo kama sheria Namba 13 ya maadili ya Viongozi
wa Umma ya mwaka 1995 inavyoelekeza.
'Ngd zangu Waheshimwa Madiwani lazima mfahamu kuwa suala la Maadili
na Utawala Bora ni jambo linalopewa nafasi ya pekee katika Serikali
yetu na ili kufikia mafanikio ni muhimu kwenu kuwa na maadili mema
ikiwa pamoja na kuwa karibu na jamii hii itaongeza ufanisi katika
utoaji wa huduma bora na watumishi wa serikali wawajibike kwa wananchi
na vyombo vya habari visaidie ili jamii nayo iwe katika
Uadilifu...Alimalizia Ulega.
Akifunga Mafunzo hayo Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Umma,Jaji mstaafu Salome Kaganda alieleza kuwa Mafunzo hayo
yameendeshwa chini ya mradi wa Elimu kwa UMMA Unaofadhiliwa na
Shirika la kutoa Misaada la Kimarekani(USAID)na kuwezeshwa na
Sekretarieti ya Maadili ya Umma alibainisha kuwa Kuongezeka kwa
Halmashauri na Madiwani na kufikia Halmashauri 162 na kuwa na Madiwani
4461 ni Baadhi ya Changamoto kwa kutoweza kuwafikia kutokana na ufinyu
wa Bajeti hali iliyofanya Halmashauri hiyo kutopatiwa mafunzo hayo
toka mwaka 2006.
'Kwa kumbukumbu zangu semina ya kwanza kwa wilaya ya Kilwa ilifanyika
mwaka 2006 na semina ya pili mwaka 2009 hii inamaanisha madiwani
waliochaguliwa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa madiwani hao hawajapata
uelewa kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa utoaji wa Tamko la Mali kwa
Viongozi wa Umma kwa hiyo naomba Ushirikiano kwa Halmashauri kusaidia
kuwezesha utoaji wa Elimu ili kutatia baadhi ya Changamoto isije
kutokea Diwani au kiongozi wa Umma akapoteza sifa za kuwa
Kiongozi..Alibainisha Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Kufuatia Mafunzo hayo ya Siku Moja yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Jumba la Maendeleo wilayani Kilwa Baadhi ya Madiwani akiwemo wa Kata
ya Miguruwe,Mitole na Lihimalyao wilayani Humo waliiomba Serikali
kubadili Sheria hiyo kwa kuongeza na Watumishi wa Umma kufuatia
Kuongezeka kwa Ubadharifu Huku Sheria ya Kutowabana na Kama Viongozi
wa Umma huku wakiendelea kijilimbikizia mali muda mfupi baada ya
kuanza kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...