UONGOZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA UNAPENDA KUWAJULISHA WADAU WA SHERIA NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KUWA, MAHAKAMA NI MOJA KATI YA WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA ALMAARUFU KAMA ‘SABASABA.’
KATIKA MAONYESHO HAYA MAHAKAMA YA TANZANIA INAKUSUDIA KUTOA ELIMU JUU YA TARATIBU MBALIMBALI ZA KIMAHAKAMA, PAMOJA NA KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHISHO MALALAMIKO YA WANANCHI WATAKAOPATA FURSA YA KUTEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA.
HUDUMA HIZO ZINATOLEWA KWENYE BANDA LA MAHAKAMA, LINALOPATIKANA KATIKA UKUMBI WA BENJAMIN MKAPA ULIOPO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA.
NJOO UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO WEWE MWANANCHI ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.
WOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
MAHAKAMA YA RUFANI (T).


Ni MUHIMU MAHAKAMA kama Taasisi kushiriki ktk Maonyesho licha ya Mtazamo wa kuwa pana dalili za Biashara ktk maonyesho hayo.
ReplyDeleteIleweke ya kuwa bila SHERIA KUSIMAMA huwezi kufanya biashara kwa kuwa baadhi ya Biashara zitahitaji Mikataba ambayo ni sehemu ya Sheria na masuala ya Mahakama.
''ENFORCING BUSINESS CONTRACTS''
Hebu fikiria ufanye biashara halafu yakukute matukio kama haya hapa chini:
1.Umekopesha mtu ktk Biashara yako kwa Mkataba akakiuka makubaliano ya kulipa.
2.Mdeni wako anatoroka na fedha zako za biashara.
3.Unafanya biashara ya ubia na mtu halafu inatokea mwenzako Mbia anafariki ghafla bila maelekezo yeyote kwenye familia yake kuhusu biashara anayoshirikina wewe.
Hivyo Mahakama haishiriki kwa minajili ya Kibiashara isipokuwa inashiriki kama Mdau wa Masuala yaHuduma za Kisheria ambazo ni Mhimili ktk harakati zote za Kibiashara!