Dkt Frateline Mlashani Kashaga wa Helsinki,  Finland,  ni mdau wa siku nyingi wa blog ya jamii katika nchi hiyo ambayo Globu ya Jamii ilizaliwa mwaka 2005. Tangia April, 2008 mpaka mwaka huu 2013 amekuwa kwenye masomo ya PhD in Social Policy , University of Helsinki, Finland . Juzi tarehe 20th June, 2013 aliweza kutetea andiko lake la  PhD public defense katika Ukumbi wa Auditorium XII Main Building of the University of Helsinki. Globu ya Jamii inampongeza kwa fanaka hiyo. HONGERA SANA SANA!
 Picha ya kwanza, ni Mdau wa Helsinki, Mr. Dennis Londo akimpongeza Dr. Frateline Kashaga mara baada ya kumaliza kutetea nondozzz yake ya PhD  katika ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.
 Mdau FRATELINE MLASHANI KASHAGA (PhD) akipongezwa na mai waifu  wake kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana mdau Dr. Kashaga, kwa kazi nzuri. Jiina lako nalifahamu sana, kutoka humo mitandaoni.

    Kwetu wanataaluma, majukumu yetu ni kuendelea kuchangia taaluma, maisha yetu yote. Nami napenda kukuhamasisha kwa hilo.

    Nafurahi kujua kuna waBongo pande hizo. Chuo Kikuu cha Helsinki nakifahamu kiasi. Nilitoa hapo mhadhara mwaka 1991. Mwezi Agosti huu nitakuja kutoa mhadhara Chuo Kikuu cha Turku.

    Nitafurahi kama tutaweza kukutana waBongo walioko huko, tujadili masuala ya taaluma, mstakabali wa nchi yetu na mambo mengine.

    Narudia tena, hongera sana Dr. Kashaga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...