Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2013

    Bado kuna wizi mkubwa unaofanywa na wanaohusika na ulinzi pale uwanjani.
    Unakuta mtu anaweza kuingia na tiketi ya elf 3 au elf 5 ukamkuta kaenda kukaa kwenye sehemu ya waliotoa 15000-20,000 yaani VIP!!.Kinachofanyika ni kuwahonga maaskari kwenye mageti na hatimae mtu anaruhusiwa kwenda jukwaa atakalo.Matokeo yake unashangaa kule VIP kumejaa hadi njia ya kupita hamna wakati tiketi huwa zinauzwa kulingana na idadi ya viti!

    Watz sijui lini tutabadilika,magumashi na ujanjaujanja kila sehemu!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2013

    Pamoja na hayo mapato yoooote magari yanakuja kubebwa kwa kushindwa kulipa madeni ya sekta zinginezo. Acheni kutia aibu na kuzitumia vibaya hela za mapato ya TFF

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2013

    Wizi wa wazi kabisa, uwanja una uwezo wa watazamaji 60000, takwimu mnazotoa waliingia watazamaji 57203? wakati uwanja ulijaa mpaka watazamaji tulikosa viti tukaketi kwenye ngazi. nina imani kubwa kwamba hata tiketi ziliandaliwa nyingi kuliko uwezo wa uwanja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...