Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassary (mwenye sururu) akichimba mtaro wa kupitisha mabomba ya Maji wakati akishirikiana kwa vitendo na wananchi wa kijiji cha Maroroni kata ya Maroroni,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.Mh. Nassary ameshirikiana na wananchi hao kwenye kazi hiyo ambayo aliiongoza vyema kabisa.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassary akiongoza vijana wa kata ya Maroroni kuchimba mitaro ya maji. Kazi hii ilianza saa Tatu Asubuhi na kumalizika saa 10 jioni.
Mbunge wa Arumeru Mashariki akikagua roller za maji katika kijiji cha maroroni kata ya maroroni baada ya kuongoza wananchi kujitolea Nguvu kuchimba mitaro ya maji. Roller hizi ni jitihada za mbunge katika kutatua kero kubwa ya maji kijijini hapo. Kulia ni mwenyekiti wa kijiji baada ya kukabidhiwa.
Kama kazi ndio hivi basi msichague wabunge wazee. Kushika sululu unahitaji kijana
ReplyDeletehaya ndito mambo tunategemea kuona,sio viongozi wanaenda kukagua kazi na suti na viatu vya mchuchumio wakati wapiga kura wnatokwa jasho,waonyeshe vitendo,ina maana kubwa sana hata kama ni kazi ndogo tu imefanyika,inawatia moyo na kuonyesha kweli 'mpo pamoja'.Safi sana.
ReplyDeleteMnaona faida ya wabunge vijana? kazi kwa kwenda mbeele bila wasi wasi. safiiiiii sana. sururu,jembe,vyoote vinahitaji nguvu changa.
ReplyDelete