MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani. Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali duniani.


Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.

Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani. Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika katika sehemu mbili.

Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja. Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa.

Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza. “Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali.

Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana.

Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.

Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.

Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ndicho walichukutuma wapiga kura wako? kama wanaufahamu mzuri basi hawatakiwi kukupa tena KURA 2015!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2013

    Zittho ni Jembe hata dunia inamtambua ila nyumbani wanamuona kama katuni fulani.Goodluck Zittho i know you from grassroot.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2013

    Sio Kuhudhulia, ni Kuhudhuria

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2013

    Ivi wewe mnyalu unafuatilia habari za zito kabwe??au unakurupuka tu kama mnyalu, tena mnyalu kwelikweli....kama kuhusu wapiga kula wa zito mbona kitambo tu alishawaomba ridhaa yao kwamba hatagombea wewe hili unalifahamu??Alafu mnyalu kua nje ya jimbo kwa kipindi cha majuma mawili kwa mtu mwenye kujua majukumu yake kama zito hakuto athiri chochote jimboni kwake.Zamani tulipokua wadogo mtu akikuita mnyalu lazima upigane.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2013

    Mnyalu inaelekea unachuki binafsi na Zitto na bila shaka umeshashindwa sana kimya kimya sasa unabwatuka!



    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...