Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa kwanza kulia) akiwa na Mwakilishi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emmanuel Ole-Naiko (wa pili kushoto)  kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipokuwa wakimsubiri Makamu wa Rais wa Botswana, Mhe. Ponatshego Kedikilwe kuwasili nchini. Mhe. Kedikilwe ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Juni had 01 Julai, 2013.
Mhe. Kedikilwe akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mhe. Membe akimkaribisha nchini Mhe. Kedikilwe mara baada ya kuwasili.
Mhe. Kedikilwe akikagua Gwaride la Heshima.
Mhe. Kedikilwe na Mhe. Membe wakifurahia burudani iliyokuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi.
Mazungumzo yakiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2013

    Ole Naiko ni wa Tatu kushoto (sio wa pili kushoto)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2013

    Samahani unamaanisha wa tatu kulia, au unasema wa tatu kushoto picha ya kwanza juu. Kama jibu ni ndiyo, hakuna kosa hapo. Ni kama vile ubishi wa glass ni half empty au half full. Nawasilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...