Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
Mkaazi wa majengo mjini Moshi aliyefahamika kwa jina la Frank Ngowi usiku wa kuamkia leo amaenusurika kifo baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace
(daladala) lenye namba za usajili T352 AFM ikifanya safari zake kati
ya Kiboriloni na katikati ya mji wa Moshi.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 3 usiku eneo la majengo polisi
jirani kabisa na zahanati ya Kishamba.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa dereva wa daladala
hiyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alionekana
amelewakupita kiasi.
Mashuhuda walidai dereva huyo baada ya kugundua amesababisha ajali
alikimbia na kuelekea maeneo ya majengo sekondari ambapo waendesha
bodaboda walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata na kumrudisha mpaka
kwenye eneo la ajali.
Askari polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kumchukua dereva wa
gari hilo pamoja na majeruhi kwa ajili ya hatua za awali.
Huu ndio usafiri aliokuwa akiutumia Bw Ngowi.
Hii ndio daladala iliyosababisha ajali na dereva wake akakimbia. Hata hivyo jitihada zilifanyika na kufanikiwa kukamatwa na kurudishwa katika eneo la ajali..
Majeruhi wa ajali Frank Ngowi aliyegongwa na daladala wakati akiendesha baiskeli akionesha majeraha baada ya kupata ajali.
Askari polisi wanawasili eneo la tukio
Baada ya dereva wa Hiace kukimbia vijana walimkimbiza na kumrudisha kwenye eneo la ajali. Picha na Dixon Busagaga


Mdau wa Magu
ReplyDelete. Waendesha baiskeli huwa wanajipitia kokote barabarani wanakotaka kwavile hamna mafunzo rasmi kabla hawajaingia barabarani.
. Vifaa vya kuakisi ( reflector ni adimu katika baiskeli zakibongo. Hamna kabisa katika baiskeli.
. Waendesha baiskeli wanakaa foleni na mstari mmoja na magari, ukipiga honi ni wakali.
. Spidi ya baiskel na gari ni tofauti bado wanalazimisha wapangane na mgari katika spidi bila kupisha.
RASTA VIPI UNATUANGUSHA MAN, HUO MKONO WAKO WA KULIA MBONA UNAONYESHA UNATAKA KUTENDA JAMBO AMBALO NI TOFAUTI KABISA NA NIA YA KUMAKATA DEREVA NA KUMRUDISHA ENEO LA TUKIO. SISI NI WATU WA MUNGU NA WEMA SIYO HAYO UNAYOTAKA KUFANYA HAPO KAMA PICHA INAVYOONYESHA.
ReplyDeleteRASTA, MFALME SELLASIE HAKUFANYA HAYO.
ReplyDelete