Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwaasa  juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo hazijengi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.

Waumini wa kanisa katoliki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokuwa wamekusanyika "Emaus Centre" Ubungo kwa ajili ya ibada ya kupanda mbegu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni. Picha na Hamza Temba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2013

    ankali naona nawewe unahamia humu au unataka kuhamia maana naona habari zinazoongoza humu ni hizi za hawa watu wa moshi mweusi au wengine hawana shughuli zinazoendelea kila ijumaa ukaweka na wao pia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...